Jumatano, 26 Aprili 2017

UTUNZAJI WA VIFARANGA(KUKU WA KIENYEJI NA WA MAYAI)


Utunzaji wa vifaranga:- siku ya kwanza waweke katika brooder(banda la kuku)wape glucose kwa masaa sita hadi nane ya kwanza kurudisha nguvu iliyo potea
baada ya kuwapa glucose wape Esb3 au S-dime au amprolium kwa siku 1-3
Siku ya 3-5 wape chick formula,Siku ya 6 wape maji peke yake,siku ya 7 wape NCD vaccine(New castle)kwa muda wa masaa 2 tu kasha wape maji yenye vitamins,siku ya 10 wape chanjo ya gumboro,siku ya 13 wape typhoprim na neoxyvital kwa muda wa siku 7 kisha wape vitamin na dawa hizi kila mwezi kwa siku tatu
b)Utaratibu wa kuwapa chanjo:- siku ya 7 wape new castle,siku ya 10 wape chanjo ya gumboro,siku ya 21 rudia kuwapa chanjo ya gumboro,siku ya 42 rudia new castle kasha rudia kila baada ya miezi 3
c)Minyoo:-Wape dawa ya minyoo wanapo fikia umri wa wiki 8 na rudia kila baada ya miezi 3
d)Magonjwa:- Chunguza tabia ya kuku kama wanakula vizuri na wanakunywa maji vizuri na ya kutosha, wanatembea vizuri na wanachangamka sikiliza sauti zao angalia mwenendo wa ukuaji wao na mwenendo wa utagaji angalia kila siku vifo vinavyo tokea bandani,ukiona mabadiliko yasiyo ya kawaida mwone mtaalam wa mifugo aliye jirani na ulipo
Upatikanaji wa vifaranga:-
Magonjwa ya kuku:- Occidiosis ugonjwa wa kuharisha hutokana na uchafu bandani au mazingira yanayo zunguka banda,wasambazaji wa ugonjwa huu ni kunguru(mwewe)ndege wanao kuja eneo lenye kuku ,panya n.k
Kutibu ugojwa huu wape amprolium au dawa ya typhoprim na neoxyvital(vijiko 2 vya chakula kwenye maji yenye ujazo wa lita 20 kwa siku 14
Kuku wanapo ambukizwa coccidiosis ni rahisi kupata typhoid ukigundua kuku wako wameambukizwa (wanaugua typhoid )wape typhoprim 30% pamoja na ctc20% au otc 20 na vitamin amilyte
Chakula kilicho tengenezwa kutumia dagaa na samaki kinachangia kuongeza kusambaa kwa ugonjwa wa typhoid kwa kuku,epuka kuwapa kuku chakula chenye samaki na dagaaa,wape maharage ya soya au mashudu ya alizeti,kuku wakiwa wanachechemea(miguu kukosa nguvu) ni kutokana na upungufu wa chokaa
Kuku wanao anza kutaga:-wape typhoprim30% na neoxyvital siku 5-7
Usafi wa banda
Baada ya kubadilisha maranda au pumba za mpunga zilizopo kwenye banda ongeza pumba za mpunga pindi ukiona zime anza kuwa chafu ugojwa ukiendelea muone mtaalam wa mifugo aliye karibu yako

MPANGILIO WA CHAKULA CHA KUKU WA KIENYEJI
Kuku wa kienyeji wanafugwa kwa sababu hutupatia kitoweo na pia hutupatia mayai na kipato kwa familia na maranyingi vifaranga wa kuku wa kienyeji hufugwa kama vifaranga wa kuku wa mayai na wa nyama
Vifaranga wenye umri wa kuanzia siku 1 hadi wiki 3-4 asipewe chick starter
Kuku wenye umri wa wiki nne huitwa mitemba kuku wa umri huu wanahitaji chakula maalum,kuanzia wiki 5-8 wapewe chick mash kuanzia wiki ya 9-17 wapewe growers mash mabadiliko yasifanyike ghafla changanya chakula cha kukuzia na kutagia.Pia unaweza kuwapa mtama mweupe au uwele na mashudu ya alizeti kutokana na kupanda kwa bei za chakula.
UJENZI WA BANDA LA KUKU(BROODER)HADI MIEZI MIWILI
Banda lenye uwezo wa kulea vifaranga 100
Banda liwe na urefu wa futi 10 upana futi 10
Kutoka msingi hadi kufikia madirisha(ventilation space)kozi nne jengea wavu wa kuku kwa ajili ya hewa urefu wa kwenda juu uwe mita 1 pia unaweza kujengea mabanzi
Urefu wa banda kwenda juu usupungue futi 10
Paa lake liwe imara lisilo vuja
Sakafu iwe imara
Mlangoni tengeneza kikaro kidogo kwa ajili ya kuweka dawa ya kuzuia magonjwa(disinfectant).
KUWEKA MARANDA AU PUMBA ZA MPUNGA
Weka ujazo wa inchi 2 katika banda la kulea vifaranga
VIPASHA JOTO NDANI YA BANDA
Tumia umeme hakikisha bulb ipo katikati zina takiwa ziwe mbili zenye W 100,umeme ukikatika tumia kandili 2 au 3 kubwa.Pia unaweza kutumia jiwe la mkaa weka juu ya tofali la nchi 5 tumia mkaa usio toa cheche na usio isha haraka .
Siku 4 au saba kabla ya kuingiza vifaranga andaa mambo yafuatayo
Kung’utia dawa ya kuua wadudu(viroboto au utitili
Tandika makaratasi au magazeti juu ya maranda
Kwenye madirisha hakikisha unaweka mapazia ya viroba au yasiyo shika vumbi
Hakikisha umeandaa pesa za kununulia chakula cha kuku,vyombo vya kunyweshea na kulia chakula pamoja na madawa.
MADAWA:-

OTCPLUS20%(KUKAUSHIA VITOVU)
VITAMIN(KUONGEZA VITAMIN)
GLUCOSE(KUONGEZA NGUVU HARAKA)
VIPIMO:-Dawa zote ,chukua maji safi na salama lita 5 kila dawa chota kijiko cha chai(grm5)weka kwenye lita 5 za maji kwa siku 5 watakunywa mchanganyo huo baada ya siku 5 wape maji safi na salama(bila dawa)
KUPOKEA VIFARANGA:- Masaa 12 kabla ya kupokea vifaranga hakikisha brooder lina joto la kutosha ili vifaranga wafikie katika joto zuri
Hakikisha umechanganya dawa zilizo tajwa hapo juu pia umeandaa chakula
Wanapo fika vifaranga hakikisha wameanza kunywa maji yenye dawa baada muda kidogo wape chakula(kumbuka kuwachanja kabla ya msimu wa mvua na baada ya msimu)
MAHALI PA KULALA KUKU WAKATI WA USIKU(PERCH-SPACE)
Kuku wapatiwe sehemu ya kulala au kupumzika
KINGA YA MAGONJWA(VACCINATIONS)
Wapewe new castle vaccine siku ya saba
Wapewe gomboro siku ya kumi na nne
Wapewe Fowl pox(ndui)baada ya wiki 8
Wapewe dawa ya minyoo mwanzoni mwa msimu wa mvua na mwishoni mwa msimu wa mvua
Usafi ni muhimu
Tanbihi:-Ni vyema kuhifadhi kumbukumbu kila unapo wapa chanjo
KUPANDA NA KUSHUKA KWA JOTO:-

Utakapo ona vifaranga wame samba punguza joto bandani
Na utakapo ona vamejikusanya ongeza joto bandani
MEDICATION

(Kutibu):- matibabu huwa baada ya uchunguzi wa daktari wa mifugo(vet officer)
Njia za kutibu:-kuwapa kwenye maji(make a cream)
Kuwapa kwenye chakula(make a premix)
Kwa njia ya kuchoma sindano(wing wabe),breast muscles(intramuscle)
Kupuliza(spray method)
Vifaranga hukoma kuwa vifaranga wafikiapo wiki nane

NJIA BORA NA YENYE KULETA TIJA KWA WAFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI
Kuchagua kuku wa kufuga:-aina za kuku wazuri-kuchi na bukini hutaga na kuatamia mara 10 kwa mwaka,hutaga kwa wingi na kwa haraka na wana faida kubwa na mtaji wake ni rahisi kwani unaweza kuanza na jogoo 1 na koo(tetea) 1au 2 na ili kuleta tija una shauriwa kuwatunza kuku vizuri
Ushauri:-mfugaji asiwaa chie kuku kuzurura sana(itasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya kuambukizwa na kuku wa jirani,mfugaji aweke uzio japo kidogo na si lazima shamba lote.Mfugaji anatakiwa aongeze vifaranga vitakavyo kua kwa kulea vifaranga mwenyewe
Dawa za kupuliza kwenye banda la vifaranga ni servin powder au akheri powder

Aina ya Vyakula Kiasi(kilo)

Magimbi,mihogo,mahindi au uwele(paraza) 40kg
Pumba za mahindi,uwele,ngano au mpunga 27kg
Mashudu ya alizeti,pamba ufuta,karanga,nazi,soya au mawese. 20kg
Unga wa mifupa,chokaa au magamba ya samaki baharini yaliyo sagwa 2.25kg
Dagaa au mabaki ya samaki
Chumvi ya jikoni 0.50kg
Virutubisho(premix) 0.2.5kg
jumla 100kg

Makadirio ya mahitaji ya chakula kwa siku kulingana na umri
umri Kiasi(grm)
Wiki ya kwanza

1 12-15
2 15-21
3 21-35
4-7 35-50
8-15 55-60
Mchanganyiko wa chakula cha kuku wanao kua na kutaga
kg kg kg kg
Malighafi inayotumika 1 2 3 4
Mahindi yaliyoparazwa 45 20
mtama 5 30
mihigo 20 10 40
Pumba za ngano 15 15 10
Pumba za mahindi 15 15 15 20
Mashudu ya alizeti 16 16

Mashudu ya pamba 3 5
Maharage/kunde zilizo sagwa 1 5 3.5 1
kisamvu 4.75
Lusina/lusani iliyo sagwa 1 5 5 2
chokaa 5 6 4 5
Dagaa au sangara 6 5 5
Mifupa iliyo sagwa 2.25 2.25 2 2
Damu iliyo kaushwa 1 5 3.25
Chumvi ya kausida 0.50 0.50 0.50 0.50
Vitamin/madini(premix 0.25 0.25 0.25 0.25
jumla 100 100 100 100

3 comments:

  1. Vifaranga wangu wana siku Tisa ni Croiler chakula nawapa energy .wamepatwa Na tatizo LA kuishiwa Nguvu miguu Na kushindwa kuinuka kabisa tatizo hapo ni nini,chakula au nini sielewi naomba ushauri

    JibuFuta
  2. Hilo ni tatizo la ukosefu wa madini ya calcium,ambayo yanafanya mifupa ikomae. JItahidi kuwapa taka za dagaa zitawasaidia. Karibu kamembakilimo kwa maendeleo yako

    JibuFuta
  3. mnafanya vizuri kutusaidia sisi tunaotamani kufuga tulikuwa hatujui jinsi ya kuanza

    JibuFuta