• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kilimo. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kilimo. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 8 Februari 2022

kilimo cha ngano na faida zake

 

kilimo cha ngano na faida zake



Utangulizi:

Hapa nchini, zao la ngano linalimwa zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Manyara, kwa upande wa kaskazini na Iringa, Mbeya na Rukwa kwa upande wa kusini. Ngano ni zao la tatu la umuhimu la chakula hapa nchini. Bidhaa mbalimbali za chakula zinazotengenezwa na ngano ni Pamoja na mikate, biskuti, keki, chapati, mandazi, n.k.


Faida za kilimo cha Ngano:

1. Mbegu yake hutumika kama chakula

2. Zao la ngano ni zao la kibiashara hivyo huongeza kipato kwa mkulima

3. Unaweza ukaongeza thamani kwa kuchakata ngano na kutengeneza bidhaa mbalimbali

4. Husaidia kwenye kilimo mzunguko hivyo kutunza virutubisho kwenye shamba


Udongo:

Ngano ni zao linalostawi vizuri katika udongo;

1. Unaopitisha maji vizuri na wenye wastani mzuri wa kiasi cha pH kati ya 5.5 mpaka 6.5.

2. Wenye unyevu wa kutosha

3. Wenye virutubisho vya kutosha vya madini kama nitrogen, fosforasi na calicium


Zao la ngano hustawi vizuri katika maeneo ya miinuko (wastani wa mita 1,200) kutoka usawa wa bahari, maeneo ya kati (usawa wa mita 900) na maeneo ya chini ya mita 900 kutoka usawa wa bahari. Hakikisha unapima udongo wa shamba lako kabla ya kuanza kilimo ili ujue afya ya udongo. Hii itakusaidia kujua ni aina gani ya mbolea utahitaji na kwa kiasi gani. Kufanya hivi kutachangia kuongeza ufanisi na upatikanaji wa mavuno mazuri.


Mbegu

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za zao la ngano zinazotumika hapa nchini. Aina hizi za mbegu zimethibitishwa na kufanyiwa majaribio na vituo vya utafiti wa kilimo hapa nchini na kuthibitika kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali. Katika kuchagua mbegu bora ni vizuri kuzingatia sifa zifuatazo;

1. Mbegu zinazozaa vizuri

2. Mbegu Zinazowahi kukomaa shambani

3. Mbegu zinazovumilia ugonjwa

4. Mbegu zinazovumilia ukame


Miongoni mwa aina za mbegu zinazofanya vizuri ni pamoja na Juhudi, Lumbesa, Sifa, Tai, Mbuni, Merina, Ngoli, Shangwe, Trophy, Selian 87, Njombe 7 na Mamba.

Mbolea:

Kiasi cha juu cha kilo 50 za mbolea za chumvi chumvi zinaweza kuhitajika katika eneo la ekari moja. Unaweza kuchanganya mbolea ya chumvi chumvi na samadi ili kuongeza ufanisi. Zipo aina mbalimbali za mbolea za chumvi chumvi. Pia unaweza kutumia mboji kurutubisha shamba lako. Ain ana kiasi cha kutumia itategemea na majibu ya vipimo vya udongo katika shamba lako.


Viuatilifu

Magonjwa na wadudu wanaweza kushambulia mimea ya ngano ikiwa shambani. Unashauriwa kukagua shamba lako mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya mimea yako. Endapo kutatokea ugonjwa au wadudu ni vema ukamuona mtaalaamu wa kilimo kwa msaada Zaidi ya utambuzi wa ugonjwa au aina ya wadudu waliopo na hivyo ukapatiwa ushauri wa aina na kiasi cha kiuatilifu cha kutumia ili kudhibiti tatizo hilo.



Mavuno:

Kiasi cha mavuno hutegemea na aina ya mbegu utakayotumia. Endapo utazingatia matunzo mazuri, unaweza kuzalisha kiasi cha 3.5 mpaka 5.5 tons/hecter.

Jumatano, 26 Desemba 2018

KUWA MILIONEA KWA KULIMA TANGAWIZI


Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China.


Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama chai, soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).


AINA ZA
TANGAWIZI 

Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo
hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica)
na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.

TABIA YA MMEA 
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi,
wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia
na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo
kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni
membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua
ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

HALI YA HEWA NA
UDONGO 
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya
kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji
mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25.
Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.

MMEA WA TANGAWIZI

UPANDAJI 
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande
vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika
urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya
tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700
cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi
inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha
sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza
kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima
kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi
au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa
uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale
kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua
magugu, kama simazine au round up hutumika.

Magonjwa na
wadudu: 
• Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta
zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp
• Mizizi fundo; inasababishwa na
Meloidegyne spp.

UVUNAJI 

Tangawizi huweza
kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 6-10 baada ya kupanda, wakati majani yake
yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa
kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa
kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo
hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao,
mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza
kupatikana.

USINDIKAJI 

Tangawizi
ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi
iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine
huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa
mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa
zimechanganywa na sukari na/au chumvi au bila kuweka kitu chochote. Hata hivyo
tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.

GHARAMA ZA
UZALISHAJI NA MAPATO


Gharama ya hekari moja

Kukodi shamba Tshs.=100,000/=

Mbegu 200, 000/=


Kulima 100,000/=

Kupanda 100,000/=

Kupalilia x 4 @ 90,000/= jumla = 360,000/=

Mbolea / samadi 150,000/=

Jumla 1,010,000/=

Mapato kwa hekari.

Ekari moja ya maandishi inatajwa kutoa kilo 8,000 hadi 10,000. Katika hali halisi, kwa uzoefu wangu, ekari moja hutoa kati ya kilo 4000 hadi 6,000. Kutegemeana na kama umeandaa shamba kwa wakati, umefanya palizi kwa wakati, uwepo wa mvua za kutosha na hali ya rutuba ya shamba lako.

Ghalama hizi hutegemea sana na msimu zinaweza shuka au kupanda zaidi.





MASOKO





Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg.





Kwa masoko ya Tangawizi wasiliana nasi kwa simu namba 0675 117 151, nasi tutakutafutia msoko ya uhakika.



Ijumaa, 21 Aprili 2017

FAHAMU KILIMO BORA CHA MIHOGO CHENYE TIJA

Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani.

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO
Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
Naliendele Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Kiroba
Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9toka ipandwe.

Mbinu bora za kilimo cha muhogo
Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:

  1. Kufyeka shamba

  2. Kung’a na kuchoma visiki

  3. Kulima na kutengeneza matuta

  4. Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda

  5. Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.

  6. Upanadaji

  7. Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:

  8.  Kulaza ardhini (Horizontal)

  9.  Kusimamisha wima (Vertcal)

  10. Kuinamisha ( Inclined/Slunted)


Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.

Palizi:

  •  Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.

  •  Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.

  • Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.

  • Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.



Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

Usindikaji bora
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:

  • Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji

  • Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo

  • Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.


Njia bora za usindikaji

  • Kwa kutumia mashine aina ya Grater

  • Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.

  • Kwa kutumia mashine aina ya chipper

  • Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.


Matumizi ya Muhogo

  • Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga

  • Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.

  • Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.


iii MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
Magonjwa
Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.

a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia katika muhogo
Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu  chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

Visababishi:
Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

Dalili za Ugonjwa
Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.

Kwenye majani

  • Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.

  • Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.


Kwenye shina
Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.


Kwenye mizizi

Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kamakizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.

Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.
Uambukizaji na ueneaji

Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.

Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sanahutokea wakati ugonjwa ukigundulika  katika hatua za mwanzo.

Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

Udhibiti/Kuzuia

  • ü  Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.

  • ü  Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.

  • ü  Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.

  • ü  Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.

  • ü  Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.

  • ü  Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.

  • ü  Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD

  •                                     


b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani
Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.

Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula  duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

Visababishi
Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa  kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).

Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:

  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virus

  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)

  • Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)

  • Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)


Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri
Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za
Awali za ukuaji wa jani.

Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
tokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.
Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
Sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.

Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.


Uambukizaji na uenezaji

 

  • Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida

  • hutumika kuzalishia mmea.

  • Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au

  • Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogo

  • katika nchi za Afrika na India

  • Usambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katika

  • Maeneo mapya.


UHIBITI NA KUZUIA

  • Hatua ya msingi ya uzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa Mmea ambao hauna uambukizo wowote.

  • Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile

  • Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.

  • Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD

  • inaangamizwa kwa kuchomwa moto.

  • Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>


WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU

Cassava Mealy Bug (CMB)



Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.



Cassava Green Mites (CGM)
Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.



White Scales
Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.

Mchwa
Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
Wanyama waharibifu
Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k

Udhibiti/Kuzuia
Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
ü  Kutumia dawa za kuulia wadudu
ü  Kutumia wadudu marafiki wa wakulima
iii Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.

Ijumaa, 14 Aprili 2017

KILIMO CHA BAMIA


 BAMIA
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.

Urefu wa mmea huwa kati ya meta moja na mbili. Matunda yake hufikia urefu wa sentimeta 10 hadi 20, na huchumwa kabla hayajakomaa sana na hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Majani yake huchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

Ustawishaji: Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

Kupanda: Kwa kawaida mbega za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.

Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini. Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondo ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka. Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

Magonjwa: Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

Jumatano, 22 Machi 2017

JINSI YA KUONGEZA RUTUBA KWENYE SHAMBA LAKO

Ili kuvuna mazao mengi lazma udingo unao lima uwe na rutuba ya kutosha ili kusababisha mazao yako kupata virutubisho muhimu kwa ukuaji
zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia mkulima kuongeza rutuba kwenye shamba lako

  usipande mazao ya aina moja kwa mfululizo, hautakiwi kupanda mazao ya aina moja mfano mahindi na mtama kwa kufuliuliza ili kuepusha virutibisho kupotea vyote  na itasababisha magonjwa na wadudu kuwa wengi shambani

usitumie mbolea za kemikali mara kwa mara,hii pia haitakiwi, mbolea za kemikali mfano UREA hua hazitajkiwi kutumika mara kwa mara husababisha alzi kupunguza rutuba mbolea hizi utumika mara moja moja zinapo itajika.

usipende sana kuchoma shamba, unapo choma shamba unasababisha kuuwa wadudud wanao sababisha kuongeza rutuba kwenye udongo na pia huua uoto asiri.

zika mabaki ya mazao baada ya kuvuna, unapo vuna mabaki ya mazao mfano mabua yanapo zikwa na kuoza husababisha kuongeza rutuba kwenye udongo husika.

panda mazao ya jamii ya mikunde, pia mazao ya mikunde mfano kunde na maharage husaidia kuongeza naitrogen ambayo inatakiwa sana na mimea hivo rutuba huongezeka

weka mbolea ya samadi ,hii ni mbolea hasiri inayo yani ni kinyesi cha ng'ombe hivo ili kuongeza rutuba inabidi uweke sana samadi kwenye shamba lako hii itasaidia sana kurudisha rutuba kwenye shamba lako.

pumzisha shamba, Wakulima wengi hua hawapendi kupumzisha shamba hivo wanashauliuwa kupumzisha shamba kwa mda hii usaidia shamba kuongeza rutuba iliyo kua imepotea.

usitumie sana viuagugu,hii pia ni mbaya kutumia ke mikali za viuagugu badala yake palilia kwa jembe na badae yazike magugu ili rutuba iendelee kubaki kwenye shamba lako.

usitifue kupita kipimo, hii husababisha mmomonyoko wa udongo na pia rututba nyingi hupote kwa huo mmomonyoko

KILIMO BORA CHA VITUNGUU


KITUNGUU-ONION (Allium cepa)

Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlo
wa familia za kitanzania. Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika
matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika
katika kutengeneza kachumbari, kiungo cha mboga, nyama na
samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia
hutumika kutengeneza supu. Vitunguu huweza kutoa Tani 10 hadi 16 Kwa ekari (magunia 80 hadi 160).

HALI YA HEWA NA UDONGO UFAAO KWA KILIMO CHA VITUNGUU
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo yasiyo na mvua
nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na joto
kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa vitunguu.
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya
kutosha. Udongo unao ruhusu mizizi kupenya kirahisi, unao hifadhi
unyevu kama vile udongo wa mfinyanzi tifutifu.
Upandaji wa mbegu za vitunguu
Hapa Tanzania upandaji wa mbegu za vitunguu katika kitalu kwa
ujumla huanza mwezi machi hadi mei kutegemea na msimu wa
kilimo. Hivyo kilimo hiki hufanyika  mara baada ya mvua za masika
kubwa kuisha. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri
wa vitunguu. Kiasi cha Kilogram 1.5 hadi 2 za Mbegu Hutosha kwa ekari moja.
Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema katika kitalu. Mbegu
zinaweza kupandwa kwa mstari au kwa kutawanya katika tuta la
kitalu. Katika upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi
ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari.
Baada ya kupanda, mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye
kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota,
matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi
kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga. Mbegu huota baada
ya siku 7 hadi 10.www.kilimofaida.blogspot.com

KUPANDIKIZA MICHE YA VITUNGUU BUSTANINI
Upandikizaji wa miche ya vitunguu bustanini hufanyika baada ya
miche kukua na kufikia ukubwa wa unene wa penseli. Mara nyingi
miche hii itakuwa imesha kaa kitaluni kwa siku 40 baada ya mbegu
kupandwa.
Usichelewe kuhamisha na kupandikiza miche hii bustanini. Kwa
sababu miche mikubwa sana itaweza kutoa maua badala ya kutoa
tunguu. Na hivyo mara nyingi vitunguu namna hii hubaki na suke la
maua.
Wakati wa kupandikiza miche haishauriwi kukata wala kupunguza
majani. Miche ipandikizwe katika nafasi ya sm 30 kati ya mstari na
mstari na sm 10 kati ya mche na mche.


Upandaji wa miche bustanini unaweza kufanyika kwenye  mistari
katika matuta au kwenye vijaruba. Vijaruba vya mraba hutumika
kwenye maeneo yenye ardhi tambarare na iliyo kame ili kuhifadhi
maji baada ya kumwagilia. Kwa sehemu zenye udongo mzito na
zenye maji mengi tumia matuta yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm
15 kutoka usawa wa ardhi.
Matunzo ya bustani ya vitungu.

UMWAGILIAJI
www.kilimofaida.blogspot.com
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha
ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu.
Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) umwagiliaji
ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na
vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba.
Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu unashauriwa kupunguza
kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyo kua. Pia ni
vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya
kuvuna. Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu
ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.
Kuthibiti magugu na kupandishia udongo
Kitunguu ni zao lisilo weza kushindana na magugu. Magugu
husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza
magonjwa na husababisha kudumaa kwa vitunguu.
Katika bustani ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia
ya kutifulia kwa jembe dogo, kung'olea kwa mkono na pia kwa
kutumia madawa ya kuua magugu.
Kama unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina
kirefu ili kutoharibu mizizi na vitunguu vyenyewe, kwani mizizi ya
vitunguu ipo juu juu sana.
Kupandishia udongo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua
muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua. Hakikisha kuwa
mashina ya vitunguu vyako ndani ya udongo kama
sentimita 5. Pia kuna aina ya vitunguu ambavyo hutoa au
hupandisha tunguu lake juu ya udongo wakati vinapokua.
Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu
sana.


MAGONJWA YA VITUNGUU NA WADUDU WAHARIBIFU

WADUDU WAHARIBIFU

Kuna aina tatu za wadudu wanao haribu zao hili:

1>Viroboto wa vitunguu
Hawa ni wadudu waharibifu namba moja wa zao la vitunguu hapa
nchini Tanzania. Husababisha upotevu mkubwa wa mavuno.
Wadudu hawa huonekana hasa wakati wa kipindi cha joto.
Dalili za kugundua
Majani yaliyo shambuliwa na wadudu hawa huwa na mabaka
meupe yenye kung'aa. Katika hali iliyo kithiri majani yote hugeuka
kuwa na tabaka nyeupe au kijivu cheupe na baadaye majani
hunyauka kabisa.
Kuzuia

Mdudu huyu huzuiwa kwa kupiga dawa kama vile thiodan-35,
Parathion nk.

Ili kupunguza uvamizi mkubwa, panga upandaji wa vitunguu
mapema ili kipindi cha joto kiingiapo zao lako liwe limekomaa.

Epuka kupanda zao la vitunguu sehemu iliyo kuwa na mazao
aina ya vitunguu kama vile liksi, vitunguu swaumu, n.k.

2> funza na minyoo ya mizizi
wanakata miche .

Hawa hupigwa vita kwa kuzingatia mzunguko wa mazao
bustanini.

MAGONJWA YA VITUNGUU

a) Ukungu mweupe
Ugonjwa huu hujionyesha kipindi cha baridi iliyo ambatana na
unyevunyevu mwingi hewani.
Dalili za kugundua Ugonjwa huu

Utaona unga unga wa rangi ya zambarau katika majani.

Majani hugeuka rangi na kuwa njano na baadaye
kunyauka.

Ugonjwa huu hupenya hadi chini kwenye tunguu na
kusababisha kuoza kwake.
Kuzuia

Unashauriwa kubadili aina ya zao katika shamba lako
kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii ya vitunguu.
Kilimo cha mzunguko wa aina mbalimbali za mazao
upangwe kiasi kwamba vitunguu visipandwe eneo moja
mpaka baada ya miaka 3 kama ugonjwa ulikuwa
mwingi.

Tumia dawa za kuzuia ukungu. Hii ifanyike kabla ya
kuona dalili za ugonjwa kwenye vitunguu. Piga dawa
kama vile maneb, dithane M45, zineb ya unga, n.k.
Wakati unapoona hali ya hewa inayo wezesha kuenea
kwa ugonjwa huu (yaani baridi iliyo ambatana na
unyevunyevu mara kwa mara). Katika kipindi hiki piga
dawa kila baada ya siku sita ili kuzuia kuingia kwa
ugonjwa. Ugonjwa ukisha ingia kwenye mimea
hauzuiliki kwani hakuna dawa ya kuponyesha.

b) Ukungu wa kahawia
Ugonjwa huu unaweza kuleta madhara makubwa wakati
vitunguu vikiwa bustanini na hata wakati vikiwa katika ghala.


Dalili zake
Vikovu vya mbonyeo hujitokeza kwenye majani na baadaye
hutoa doa la rangi ya zambarau. Vikovu hivi hukua na
kutengeneza vidonda ambavyo hukua na kufanya mzunguko
katika jani zima au shina la kitunguu. Baada ya wiki kama tatu
hivi tangu kuingia kwa ugonjwa huu, majani yote huanguka na
kukauka.
Ugonjwa huu hushambulia vitunguu hata baada ya kuvuna kwa
kupitia shingo ya kitunguu au sehemu yoyote yenye kovu,
kidonda au mkwaruzo.
Namna ya kuzuia

Katika bustani, mara uonapo kitunguu chenye dalili za
ugonjwa huu, ondoa mimea na kuiteketeza kwa moto ili
kuzuia au kupunguza kuenea kwa ugonjwa.

Kwa kinga ya bustani, piga dawa za Dithane M 45 na dawa
zingine za kuzuia magonjwa ya ukungu. Dawa hizi zitasaidia
kupunguza kutawanyika  kwa ugonjwa.

Tumia kilimo cha kuzungusha au kubadilisha mazao katika
eneo la bustani yako. Usipande mfululizo jamii yoyote ya
vitunguu katika shamba ulilovuna vitunguu.

Wakati wa kuvuna, epuka kukata au kusababisha vidonda
katika vitunguu, yaani vuna kwa kung’olea na siyo kwa
kuchimba na jembe.

Baada ya kuvuna anika vitunguu juani kwa siku moja au mbili
kabla ya kuviweka katika magunia au ghala.

c) Ugonjwa wa kuoza mizizi
Huu ni ugonjwa unaotoka udongoni na unasababishwa na
vimelea vya jamii ya ukungu.
Dalili
Dalili za ugonjwa huu ni mizizi kugeuka rangi na kuwa njano na
baadaye kuwa zambarau. Baada ya muda ugonjwa huenea na
mizizi hufa kwa kunyauka. Majani nayo hugeuka kuwa na rangi
ya njano na kisha shina au mche mzima hunyauka.
Kuzuia

Tumia kilimo cha kuzungusha mazao badala ya kupanda
vitunguu katika eneo moja toka msimu moja hadi
mwingine.

Panda aina za vitunguu zinazo vumilia ugonjwa huu kwa
mfano: Excel, L 36, Granex, White Granex na red creole.
Uvunaji wa vitunguu
Kwa ujumla uvunaji vitunguu hufanyika baada ya siku 90 hadi
150 tangu kupanda kwa miche yaani miezi mitatu hadi mitano
tangu miche kupandikizwa bustanini.
Utagundua kuwa vitunguu viko tayari kuvunwa baada ya kuona
kuwa karibu asilimia 50 au nusu ya mimea shambani inaanza
kuanguka na majani kukauka.
Ili kurahisisha ukaushaji na hifadhi sahihi ya vitunguu, pangilia
vizuri msimu wa kupanda ili kwamba uvunaji ukutane na kipindi
cha joto na kiangazi.
Uvunaji ufanyike kwa kung'oa baada ya kumwagilia maji bustani
siku moja kabla ya kuvuna.
Baada ya kuvuna kata majani kama sentimeta 2 juu ya tunguu.
Pia kata mizizi mirefu kwa sm 2 (usikate chini sana ya shingo
wala kitako cha kitunguu kwani hii husababisha kuoza kwenye 26
ghala au gunia la kusafirishia na kuenea kwa magonjwa. Baada
ya hapo kitunguu kianikwe juani kwa siku 1 hadi 2.
Vitunguu vilivyo anikwa vizuri ni vigumu kwa kubonyeza kwa
kidole gumba pia shingo ya kitunguu huwa kavu.
Mavuno ya vitunguu vilivyo tunzwa vizuri yaweza kufikia tani 7
hadi 10 kwa hecta.
Baada ya kuvuna na kuanika:

Chagua vitunguu vizuri, tenga vibovu na vilivyo vidogo
sana

Ondoa vitunguu vilivyo na makovu pamoja na vile vyenye
shingo nene (shingo ya chupa).

Undoa maganda yanayo pepea ovyo.
Baada ya uchambuzi huu, hifadhi vitunguu kwenye ghala kama
husafirishi na kama unasafirisha pakia vitunguu katika magunia
yenye kupitisha hewa ya kutosha.
Katika ujazaji wa magunia usishindilie na wala usiweke
vitunguu vichache katika gunia. Kushindilia sana vitunguu
hubabisha mkandamizo mkubwa na hivyo kuoza kwa vitunguu,
na usipojaza vizuri vitunguu katika magunia hutokea msuguano
wakati wa kusafirisha na hivyo kusababisha vidonda vitakavyo
fanya vitunguu kuoza.
Kama vitunguu havisafirishwi kwa ajili ya soko, vinaweza kutunzwa
katika sehemu kavu
iliyo na mzunguko mzuri wa hewa ya kutosha.
Vitunguu kama vile aina ya Red Creole na Texas Grano
vinahifadhika vizuri. Kwa vitunguu vilivyo hifadhiwa vizuri, huweza
kudumu hadi miezi 6 bila kuharibika. Kwa sehemu zilizo na joto
kali, usihifadhi vitunguu zaidi ya miezi mitatu kwani vitunguu
huanza kuoza na au kuchipua.
Picha ya vitunguu vya Red Creole

Image result for picture of red creole onion

Picha ya vitunguu vya texas Grano

Image result for piCTURE OF TEXAS GRANO ONION