Jumatano, 26 Desemba 2018

KUWA MILIONEA KWA KULIMA TANGAWIZI


Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China.


Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama chai, soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).


AINA ZA
TANGAWIZI 

Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo
hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica)
na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.

TABIA YA MMEA 
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi,
wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia
na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo
kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni
membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua
ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

HALI YA HEWA NA
UDONGO 
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya
kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji
mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25.
Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.

MMEA WA TANGAWIZI

UPANDAJI 
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande
vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika
urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya
tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700
cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi
inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha
sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza
kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima
kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi
au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa
uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale
kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua
magugu, kama simazine au round up hutumika.

Magonjwa na
wadudu: 
• Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta
zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp
• Mizizi fundo; inasababishwa na
Meloidegyne spp.

UVUNAJI 

Tangawizi huweza
kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 6-10 baada ya kupanda, wakati majani yake
yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa
kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa
kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo
hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao,
mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza
kupatikana.

USINDIKAJI 

Tangawizi
ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi
iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine
huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa
mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa
zimechanganywa na sukari na/au chumvi au bila kuweka kitu chochote. Hata hivyo
tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.

GHARAMA ZA
UZALISHAJI NA MAPATO


Gharama ya hekari moja

Kukodi shamba Tshs.=100,000/=

Mbegu 200, 000/=


Kulima 100,000/=

Kupanda 100,000/=

Kupalilia x 4 @ 90,000/= jumla = 360,000/=

Mbolea / samadi 150,000/=

Jumla 1,010,000/=

Mapato kwa hekari.

Ekari moja ya maandishi inatajwa kutoa kilo 8,000 hadi 10,000. Katika hali halisi, kwa uzoefu wangu, ekari moja hutoa kati ya kilo 4000 hadi 6,000. Kutegemeana na kama umeandaa shamba kwa wakati, umefanya palizi kwa wakati, uwepo wa mvua za kutosha na hali ya rutuba ya shamba lako.

Ghalama hizi hutegemea sana na msimu zinaweza shuka au kupanda zaidi.





MASOKO





Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg.





Kwa masoko ya Tangawizi wasiliana nasi kwa simu namba 0675 117 151, nasi tutakutafutia msoko ya uhakika.



1 comments:

  1. Hi..,there nashukulu sana kwakunipa elimu ya kutosha katika hiki kilimo cha tangawizi. Mimi naishi zambia na huwa nafatilia sana kilimo cha tanzania hasa nikilimo cha umwagiliaji nanime vutiwa sana na kilimo cha tangawizi je katika hecta moja nikiasi gani cha mbegu

    JibuFuta