Alhamisi, 6 Desemba 2018

viatamishi (incubators)




Wafugaji wengi wanaonesha kuvutiwa na njia ya utotoleshaji wa mayai unaofanywa na mashine maalumu za kutotolesha mayai maarufu kwa jina la viatamishi (incubators) .Wengi wana kiu ya kutaka kujua gharama, faida, hasara na upatikanaji wa mashine hizi.Kwa kuthamini mchango wa wafuatiliaji wa website hii, nimelazimika kuitumia wiki hii kulielezea hili swala kwa upana wake.

.Viatamishi ni nini?   Hizi ni mashine maalumu zinazotumika kurahisisha utotoleshaji wa mayai ya aina zote  ya kuku wa asili na wale wa kisasa. Pia, inaweza kutumika kwa mayai ya kwale, bata na kanga.Mashine hizi hutofautiana ukubwa, lakini pamoja na tofauti hiyo, bado kila moja ina uwezo wa kutumia muda mfupi kutotolesha mayai, tofauti na muda anaoutumia kuku kuatamia hadi kupata vifaranga.Aina za viatamishiKwa jumla, mashine hizi zote zina kazi moja tu ambayo ni utotoleshaji, japo zimetofautishwa kwa mifumo yake ya kiuendeshaji.Mfumo wa kwanza unazijumuisha mashine zote zinazototolesha mayai kwa kujiendesha zenyewe(automatic).Mfumo wa pili unaziunganisha mashine zote zinazofanya kazi kwa kuendeshwa kwa msaada wa kibinadamu.

Mashine zinazojiendesha zenyewe zinatumika sana kibiashara kwa sababu zinarahisisha kazi tofauti na ilivyo kwa zile zinazoendeshwa na binadamu.Mashine hizi zina faida kubwa kwani si rahisi kuharibu mayai kutokana na kuwa na mashine ndani ambayo kazi yake ni kusaidia kutawanya joto kwenye mayai.Uzuri wake ni kwamba hata joto likizidi uwezekano wa kuharibu mayai haupo kwa sababu feni inasaidia kupunguza joto ndani ya mashine.Kundi la pili linajumuisha mashine zinazofanya kazi zake kwa kutumia uwapo wa mtu muda wote.Aina hii ya mashine hutumia upepo wa kawaida kuendesha zoezi la utotoleshaji, haina feni maalum lakupoza joto.Hii ina maana lazima mtu awe karibu na mashine wakati wote wa utotoleshaji ili aweze kufanikisha mchakato wote.Sifa za viatamishi Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa mashine hizi hazitofautiani sana, ukiachilia mbali ukubwa na mfumo wa uendeshaji. Zipo mashine zenye uwezo wa kutotolesha mayai mengi zaidi kwa pamoja, na nyingine kulingana naudogo wake zinalazimika kutotolesha mayai machache kwa muda mfupi pia.Kwa kawaida mashine nyingi za utotoleshaji hutumia umeme kidogo wa unaokadiriwa kuwa waVoltage:110V- 220V.Ukifanikiwa kupata mashine bora, unajijengea uhakika wa kutotolesha asilimia 95 ya mayai yote.

Unazijuaje mashine bora? Si jambo rahisi kuzijua mashine bora, lakini unaweza kutazama baadhi ya vitu muhimu kama vile tochi maalumu yenye uwezo wa kukagua uhai wa mayai yaliyomo ndani ya mashine.Zipo mashine zenye uwezo wa kila trei ya mayai kuwa na sehemu ya kuangulia vifaranga, kuangalia mfumo maalumu ‘full Automatic’ unaoweza kugeuza mayai, kudhibiti joto na unyevu ndani ya mashine.Jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha unatumia mashine yenye uwezo wa kutunza joto kwa muda wasaa sita mara baada ya umeme kukatika.

Viatamishi vya mafuta :Ni muhimu pia kueleza kuwa mbali ya nishati ya umeme, viko vitamishi vinavyoweza kujiendeshakwa kutumia nishati ya mafuta kama ya taa au petrol. Kwa kawaida aina hizi za viatamishi huwa na gharama ndogo.Kwa Watanzania na hata viwanda vidogo vimekuwa vikitengeneza aina hizi za viatamishi. Ni muhimu kutafuta taarifa za viatamishi hivi kutoka kwa wataalamu wa ufugaji au wafugaji wakubwa.



Related Posts:

  • HIZI NDIZO SABABU ZA KUKU WAKO KUDONOA MAYAI NA KUDONOANAKati ya mambo ambayo mfugaji anatakiwa kuwa nayo makini ni pamoja na tabia za kila siku za mifugo yake. Kuna wakati kuku wanakuwa na tabia za kudonoa na kula mayai,pia kudonoana wenyewe kwa wenyewe. Tabia hii si nzuri na si y… Read More
  • Mtaji wa kufuga kuku wa kienyeji, mchanganuo wake na namna ya kupata sokoPengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye… Read More
  • viatamishi (incubators)Wafugaji wengi wanaonesha kuvutiwa na njia ya utotoleshaji wa mayai unaofanywa na mashine maalumu za kutotolesha mayai maarufu kwa jina la viatamishi (incubators) .Wengi wana kiu ya kutaka kujua gharama, faida, hasara na upat… Read More
  • Black Australorp ( Kuku Weusi wa Malawi)Australorp wanastahimili mazingira tofauti, kama kuku wa kienyeji aliye zoeleka nchini Tanzania. Na ni wazuri kwa ufugaji huria, kwa kuwaachia nje wajitafutie chakula wenyewe. Ingawa wanajulikana kwa sifa yao ya utagaji mayai… Read More
  • LISHE YA KUKU NA KUCHANGANYA CHAKULALISHE YA KUKU:Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula kingi na chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa lishe ya kuku unaweza kuainishwa katika makundi ya vyakula kama if… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni