• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Afya. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Afya. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 19 Aprili 2017

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO


BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.
Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.

MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.

NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.

KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Alhamisi, 13 Aprili 2017

ATHARI ZA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA


MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA:
Matumizi na biashara ya dawa za kulevya yameendelea kusababisha madhara makubwa mbalimbali nchini yakiwemo ya kiafya, kijamii, kiuchumi, kimazingira, kisiasa na kiusalama.

KIAFYA:
Dawa za kulevya zimeendelea kuleta madhara makubwa kiafya yakiwemo magonjwa ya akili, utegemezi wa dawa za kulevya, magonjwa ya mapafu, moyo, ini na figo. Aidha, matumizi ya dawa za kulevya yaliendelea kusababisha vifo vya ghafl a hasa miongoni mwa wajidunga kutokana kuzidisha dozi. Pia, matumizi ya dawa hizo yameendelea kuchangia kuenea kwa maambukizi ya VVU, kifua kikuu na virusi vya homa ya ini aina ya B na C. Watumiaji wengi wameendelea kukabiliwa na magonjwa ya meno na ngozi yakiwemo majipu, vidonda na ukurutu. Dawa za kulevya zimeendelea kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume, ugumba, utasa na kuzaliwa kwa watoto wenye ulemavu, njiti na wenye matatizo ya ukuaji wa kiakili na kimwili. Jedwali Na.8 linaonesha viwango vya maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa watumiaji waliojitokeza kupata matibabu kwenye hospitali za Muhimbili.

KIUCHUMI:
Matumizi ya dawa za kulevya huongeza mzigo kwa taifa kwa kuwa hupunguza nguvu kazi na husababisha uharibifu wa mali. Vilevile, gharama za udhibiti zikiwemo utoaji wa elimu kwa umma, uteketezaji wa mashamba ya bangi, uendeshaji wa kesi, kuwatunza wafungwa magerezani na kuwatibu watumiaji huongeza mzigo kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Biashara ya dawa za kulevya husababisha mfumuko wa bei unaotokana na fedha za biashara hiyo kuingizwa kwenye mfumo halali. Aidha, matumizi ya dawa zakulevya husababisha utoro mashuleni au kazini, kusitisha masomo au kufukuzwa kazi. Kwa ujumla, matumizi na biashara ya dawa za kulevya vimeendelea kuchangia kuongeza umaskini nchini.

KIJAMII:
Dawa za kulevya zimeendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii. Utumiaji na biashara ya dawa za kulevya mitaani husababisha tabia hiyo kuzoeleka na hivyo kuwavutia watu wengine hasa watoto kujiingiza kwenye tatizo hilo na kuchangia kuharibika kwa kizazi kijacho.Aidha, matumizi ya dawa ya hizo huchangia migogoro ya kifamilia katika jamii jambo linaloweza kuzisambaratisha kabisa. Wazazi ambao hutumia dawa za kulevya, huonesha mfano mbaya kwa watoto wao na jamii kwa ujumla. Pia, kumekuwepo na ajali zilizosababishwa na uendeshaji wa magari na mashine huku waendesha vyombo hivyo wakiwa wametumia dawa za kulevya. Ajali hizo mara kwa mara zimekuwa zikisababisha ulemavu na vifo vingi. Wajidunga hutupa ovyo mabomba ambayo huweza kusababisha majeraha kwa wapita njia au maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Watumiaji wamekuwa wakijihusisha na tabia na vitendo viovu vikiwemo wizi, uporaji, biashara ya ngono na ubakaji. Jamii imekuwa ikiamini kuwa matumizi ya dawa za kulevya ni jambo la kujitakia, hivyo kuwanyanyapaa na kuwabagua watumiaji. Vitendo na muonekano wao huwafanya wasikubalike katika jamii jambo linalosababisha kuendeleza vitendo vyao vya uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya. Halikadhalika, kosa la kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya huambatana na adhabu kali ikiwemo kifungo cha maisha jambo ambalo linawatenga wahusika na familia zao pamoja na jamii. Biashara ya dawa za kulevya huhusisha rushwa kubwa ambayo huathiri utoaji haki kwa wananchi na utawala bora. Wafanyabishara wa dawa za kulevya hutumia sehemu ya faida wanayopata kusaidia jamii ambayo huwaonea aibu kuwachukulia hatua pindi wanapojihusisha na vitendo viovu.

Wafanyabiashara hujitumbukiza kwenye vitendo vya kihalifu kama utekaji nyara, ugaidi, mauaji ya kikatili, vita vya wenyewe kwa wenyewe na ujambazi, hivyo kusababisha uvunjifu wa amani. Vilevile, wafanyabiashara wa dawa za kulevya huweza kuwarubuni watendaji wa vyombo vya udhibiti wa dawa za kulevya kuvujisha siri hivyo kuhatarisha maisha ya watendaji na raia wema.

KISIASA:
Wafanyabiashara wa dawa za kulevya huweza kuwashawishi wapiga kura kwa kutumia rushwa kuwachagua viongozi watakaosimamia maslahi yao pindi watakapokuwa madarakani. Biashara ya dawa za kulevya huweza kuchochea machafuko ya kisiasa na kuweza kupindua serikali iliyopo madarakani. Halikadhalika, nchi inayojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya huharibu taswira ya nchikimataifa na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo raia wake kutoaminika na kupata usumbufu mkubwa wanapokuwa kwenye nchi nyingine.

KIMAZINGIRA:
Kilimo cha bangi kinachofanyika kwenye vyanzo vya maji na kwenye ardhi oevu husababisha kukauka kwa mito na kuleta ukame. Pia, ukataji miti ovyo na uchomaji moto wa misitu kwa ajili ya kuandaa mashamba ya bangi husababisha mmomonyoko wa udongo.

NB:
Kila ifikapo tarehe 26 mwezi wa 6 kila mwaka,hua ni siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya duniani.

Jumatano, 12 Aprili 2017

MADHARA YA BANGI


Bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Uko mitaani bangi ina majina mengi na watumiaji wake wameipa majina kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga.

Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa
Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish.

Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe
(hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake.Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.

Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu,maua, na mche na huwa na rangi ya kijani,kijivu au brauni na bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika sehemu nyingi duniani.

Bangi hutumika kwa kuvuta moshi kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake. Ni mara chache huchanganywa katika chakula, kuliwa kama mboga au kutengeneza kinywaji. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na watumiaji kama “blunt”

Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo katika uhalisia (ndoto za mchana/maruweruwe).Matokeo haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC kilichovutwa na ukali wake.

Mara nyingi wavutaji wa bangi huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.

Matatizo ya ubongo yanayopelekea kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.

Jumamosi, 8 Aprili 2017

Vyakula bora kwa afya ya mama na mtoto


Lishe ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto – hili si jambo geni sana. Lishe bora ni lazima kwa watoto wadogo sababu wanatakiwa kukua vizuri – kimwili na kiakili.

Je lishe bora ni ipi?

Lishe bora ni chakula chenye virutubisho vyote muhimu kwa kiasi na uwiano sahihi ili kuuwezesha mwili wa mtoto kupata siha nzuri (afya bora). Wataalamu wanachambua zaidi kwa kusema kuwa lishe bora ina virutubisho aina sita, ambayo ni: Wanga, Protein, Mafuta, Vitamin, Madini na Maji.

Je vyakula gani ni bora ?

Lishe bora inatakiwa kuwa na mboga za majani, matunda, protini, wanga na madini ya kutosha. Hizi zinapatikana kwenye vyakula aina tofauti, na kuna vyakula vingine vina virutubisho vingi kwa pamoja.

Mfano wa vyakula vyenye lishe bora kwa kiwango kinachofaa ni kama mboga za majani, mafunda, nafaka asilia, vyakula vya protini (mayai, maharage, nyama n.k) na vyakula vyenye mafuta yasiyohifadhiwa mwilini.
Watoto wanagawanywa kwenye makundi ya aina mbili : Kuzaliwa hadi miezi 6 na kuanzia miezi 6 na kuendelea. Haya makundi ni muhimu sababu watoto waliopo kwenye makundi haya wanatofautiana aina za vyakula wanavyokula. Ni muhimu kuzingatia hili sababu huu ndio muda muhimu zaidi katika ukuaji wa mtoto.

Lishe ya mtoto mchanga hadi miezi 6


Inashauriwa kuwa mtoto mchanga – tangu anazaliwa hadi afikapo miezi 6 – asipewe kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama, hii ikiwa inamaanisha hata maji ya kunywa. Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu (pamoja na maji) vinavyohitajika kwenye ukuaji mzuri wa mtoto na kumpa kinga ya magonjwa mbalimbali.

Photo by Google

Lishe ya mtoto kuanzia miezi 6


Mtoto akishafika umri wa miezi 6, anaweza kuanza kula vyakula mbali mbali. Inashauriwa mtoto aanze kupewa vyakula mbali mbali kidogo kidogo ili apate kuzoea. Vyakula hivi lazima view vimepondwa, au viwe kwenye mfumo wa uji au maji sababu mtoto anakuwa hana meno yaliyokomaa au wengine wanakuwa hawajaanza kabisa kuota meno.

Lishe ya Mama


Ukizungumzia mtoto hutoweza kuacha kuzungumzia mama. Mama ndiyo chanzo kikubwa cha chakula kwa mtoto tangu anazaliwa hadi anakuwa huru kula chakula cha kawaida. Kwa mwanamke mwenye umri wa kubeba ujauzito au mwenye ujauzito, ni muhimu kula vizuri ili kujenga afya ambayo ndio chanzo kikubwa cha virutubisho kwa mtoto tumboni na baada ya kuzaliwa. Ili kuwa na siha nzuri, vyakula vyote vinatakiwa kuwa na uwiano mzuri wa virutubisho.

Inatakiwa kuzingatiwa kuwa, vyakula vya mtoto viwe vya kuongezea lishe, lakini ni vizuri mtoto akiendelea kunyonya maziwa ya mama hadi atakapofikisha miezi 24. Maziwa ya mama ni muhimu katika kumfanya mtoto akue vizuri, hasa katika miezi 24 ya mwanzo. Inashauriwa kuwa, kama hakuna kikwazo – mfano: ugonjwa wa maambukizi unaoweza kumdhuru mtoto – ni vizuri mama amnyonyeshe mtoto kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita (6).

Faida kubwa ya kunyonyesha ni kusaidia ubongo wa mtoto kukua vizuri zaidi sababu maziwa ya mama yanatoa virutubisho kwa wingi kuliko vyakula atakavyokula yeye moja kwa moja. Hii ni kwa sababu, tumbo la mtoot linakuwa halijazoea kusaga vyakula tofauti, hivyo maziwa ni chakula kinacholeta virutubisho vinavyotumika moja kwa moja mwilini.

Umuhimu wa lishe bora


Kama ilivyoelezwa mwanzo, lishe bora ni muhimu. Zifuatazo ni baadhi ya faida apatazo mtoto anayepata lishe bora:

  • Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini na kuufanya mwili kupambana kirahisi na magonjwa kama utapiamlo (kwashiorkor) na kiriba tumbo

  • Kujenga siha nzuri (afya bora)

  • Kuleta furaha na Amani

  • Kusaidia ukuaji wa mwili na akili

  • Kuleta nguvu na kusaidia mwili kufanya kazi vizuri


Madhara ya lishe duni


Kama mtoto akiwa na lishe duni, haya yatakuwa madhara yake:

  • Kupata magonjwa mara kwa mara sababu anakosa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa

  • Kudumaa kukua mwili na akili

  • Uwezekano mkubwa wa kupata ulemavu sababu mifupa inakuwa laini na haiwezi kustahimili uzito wa mwili.

  • Upungufu wa damu hivyo kudhoofisha afya ya mtoto

  • Kupata utapiamlo (Kwashiorkor)

  • Kupoteza maisha katika umri mdogo

Alhamisi, 16 Machi 2017

JIKINGE AU JITIBU ‘PRESHA YA KUSHUKA ’ KWA CHAKULA


Presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu (hypotension) hali hii inatokea pale msukumo wa damu unapakua mdogo na dhaifu, halo ambayo husababisha viungo muhimu katika mwili (major organs) kushindwa kupokea kiasi cha damu na oksijeni kinacho jitosha

DALILI ZA MTU MWENYE PRESHA YA KUSHUKA

Mtu mwenye ugonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara husumbuliwa na uchovu, mwili kukosa nguvu, kuwa mnyonge na kusikia kizunguzungu. Hali hii hutokea baada ya mzunguruko wa damu kwenye mishipa kuwa mdogo kutokana na kupungua kwa msukumo wa damu hivyo viungo kama moyo, ubongo na viungo vingine kupungukiwa au kukosa damu kabisa.

SABABU ZA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa mujibu wa wataalamu wetu wa masuala ya lishe, sababu kubwa inayochangia ugonjwa huu ni ukosefu wa virutubisho mwilini kunakosababishwa na ulaji usio sahaihi. Mtu anapokuwa na upungufu wa protini, vitamin C au moja kati ya Vitamin B hupatwa na tatizo hili. Aidha, ugonjwa wa presha ya kushuka, wakati mwingine husababishwa na kuvuja taratibu kwa damu mwilini kupitia kwenye utumbo, figo au kibofu. Mbali na matatizo hayo, pia hasira, kupatwa na msongo wa maisha na mawazo mengi, kunaweza kusababisha presha ya kushuka pia.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa mujibu wa watatifi wa vyakula, wamegundua kuwa juisi ya Bitiruti (beetroot) ina saidia sana mgonjwa anayesumbuliwa na ugonjwa huu. Bitiruti ni aina fulani ya viazi pori ambavyo vinabapatikana kwenye masoko mbalimbali nchini. Mgonjwa anashauriwa kutengeneza na kunywa kikombe kimoja cha juisi hiyo kutwa mara mbilli na anaweza kuona mabadiliko ndani ya wiki moja tu.

KUOGA MAJI YA CHUMVI
Dawa nyingine inayoweza kutoa nafuu na ya haraka kwa mgonjwa wa presha ya kushuka ni kuoga kwa kujiloweka kwenye maji ya chumvi maalum. Chukua kilo moja na nusu ya chumvi, kisha weka kwenye beseni kubwa la maji ya uvuguvugu, koroga kisha ingia ndani ya beseni hilo na ukae kwa dakika 10 hadi 20. Fanya hivyo muda mfupi kabla ya kwenda kulala na usipatwe na baridi.

VIRUTUBISHO KAMA TIBA
Protini, Vitamin C na Vitamin zote za kundi B, vimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga au ahueni kwa wagonjwa wa presha ya kushuka. Mlo kamili wowote ulioshehemi vitamini B na virutubisho vingine, ni muhimu kuliwa na mgonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara.

Matumizi ya chumvi nyingi kwa mgonjwa wa presha ya kushuka nayo ni muhimu. Mgonjwa anashauriwa kula vyakula vyenye chumvi nyingi. Aidha, anaweza kunywa maji yaliyochanganywa nusu kijiko cha chumvi kila siku, hadi hapo kiwango cha presha yake kitakaporejea katika hali ya kawaida.

Ili kuliondoa tatizo la presha ya kushuka moja moja, mgonjwa wa presha ya kushuka anatakiwa kuzingatia ulaji wa matunda kwa kiasi kikubwa. Kwa kuanzia, anatakiwa kula mlo wa matunda-matunda tu kwa muda wa siku tano mfululizo, huku akila mlo huo mara tatu kwa siku ukipishana kwa umbali wa masaa matano.

Baada ya hapo, mgonjwa huyo anaweza kubadilisha mlo na ukawa wa matunda na maziwa kwa muda wa wiki mbili hadi tatu. Na baada ya hapo, anatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vyenye virutubisho vya kutosha ili kuimarisha mfumo wa damu mwilini. Na hii ndiyo iwe staili yake ya maisha kila siku, bila kusahahu mazoezi mepesi mepesi, yakiwemo yale ya kuvuta pumzi na kushusha.

Jumatano, 15 Machi 2017

Chakula cha mtu mwenye Vidonda vya Tumbo



Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo na leo tunaendelea kuangalia chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.

Mtu mwenye vidonda vya tumbo ni mtu mwenye asidi nyingi mwilini kuliko alkalini, hivyo anatakiwa kupendelea zaidi kula matunda na mboga za majani. Anahitaji zaidi ukijani mwilini mwake. Pia apendelee kula ugali wa dona kuliko ugali wa sembe na inashauriwa pia kupunguza kula wali.

Kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni maji. Hakikisha unakunywa kila siku maji glasi 8 hadi 10.

 

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5


Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.


Hapa chini nimekuwekea jedwali la jumla la vyakula na vinywaji vyenye asidi sana, asidi ya kati na alkalini sana, vile vya kuviepuka ni vile vyenye asidi sana, orodha itaendelea kuboreshwa;

Chakula cha mtu mwenye Vidonda vya Tumbo

Mayai na bidhaa za maziwa

  • Alkaline: mtindi

  • Neutral: mtindi mtupu (plain Yogurt ),

  • Acid: siagi, krimu, mayai, jibini ngumu (Hard Cheese), Ice Cream, jibini ya kiwandani (Processed Cheese), maziwa


Vyakula jamii ya maharage

  • Alkaline: Lima, njegere, Snap, String

  • Neutral: Soya

  • Acid: Black, Garbanzo, Kidney, dengu


Vyakula jamii ya karanga

  • Alkaline: lozi, Nazi freshi (fresh)

  • Neutral:

  • Acid: Brazil, korosho, Nazi kavu (dried coconut), Macadamia, karanga, Pecan, Pistachio, Walnut


Mboga za majani

  • Alkaline: asparaga (Asparagus), kiazisukari (Beets), brokoli (broccoli), kabeji, karoti, Koliflawa (aina ya kabichi – Cauliflower), figili (Celery), tango, mwani (Kelp), saladi (Lettuce), uyoga, vitunguu, kotimiri (Parsley), Bell Peppers, viazi ambavyo havijamenywa (with skin), boga (Squash), nyanya

  • Neutral: Horseradish, Rhubarb, Sauerkraut

  • Acid: Spinachi iliyopikwa, viazi ambavyo vimemenywa (no skin Potato), achali


Matunda

  • Alkaline: tufaa (Apple), parachichi, tende, mtini, zabibu, balungi, Kiwi, Limau, ndimu, embe, tikiti maji, chungwa, mpichi, Pears, Stroberi

  • Neutral:

  • Acid: Blueberry, Cranberry, plamu (Plum), plamu kavu (Prune)


Vinywaji

  • Alkaline: Maji ya limau, Chai ya tangawizi

  • Neutral: Maji

  • Acid: Chai ya rangi, Bia, kahawa, vinywaji vyenye kafeina, juisi za viwandani (processed), Liquor, Soda, Wine


Viongeza utamu

  • Alkaline: Asali mbichi (Raw Honey), sukari mbichi (Raw Sugar), Stevia

  • Neutral:

  • Acid: Viongeza utamu vyote vya kutengenezwa (Artificial Sweeteners)


Nyama

  • Alkaline:

  • Neutral:

  • Acid: Nyama ya ng’ombe, kuku, Samaki, mbuzi, batamzinga, nyama ya nguruwe, Sungura


Mafuta

  • Alkaline: mafuta ya mbegu za katani

  • Neutral: mafuta ya lozi, Canola, mafuta ya nazi, mafuta ya mahindi, Margarine, mafuta ya zeituni, Safflower, mafuta ya ufuta, mafuta ya Soya, mafuta ya alizeti

  • Acid:


Vitafunwa & nafaka

  • Alkaline: Amaranth, Millet, Quinoa

  • Neutral:

  • Acid: Barley, Buckwheat, Oats, mchele, Rye, Spelt, ngano, Pasta (vyakula jamii ya tambi), biskuti


Mbegu

  • Alkaline: Alfalfa (sprouted), chia (sprouted), Sesame (sprouted)

  • Neutral:

  • Acid: boga, alizeti, ngano