Jumatano, 12 Aprili 2017

MADHARA YA BANGI


Bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Uko mitaani bangi ina majina mengi na watumiaji wake wameipa majina kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga.

Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa
Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish.

Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe
(hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake.Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.

Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu,maua, na mche na huwa na rangi ya kijani,kijivu au brauni na bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika sehemu nyingi duniani.

Bangi hutumika kwa kuvuta moshi kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake. Ni mara chache huchanganywa katika chakula, kuliwa kama mboga au kutengeneza kinywaji. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na watumiaji kama “blunt”

Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo katika uhalisia (ndoto za mchana/maruweruwe).Matokeo haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC kilichovutwa na ukali wake.

Mara nyingi wavutaji wa bangi huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.

Matatizo ya ubongo yanayopelekea kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.

Related Posts:

  • Vyakula bora kwa afya ya mama na mtotoLishe ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto – hili si jambo geni sana. Lishe bora ni lazima kwa watoto wadogo sababu wanatakiwa kukua vizuri – kimwili na kiakili.Je lishe bora ni ipi? Lishe bora ni chakula chenye virutubisho vyote mu… Read More
  • MADHARA YA BANGIBangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Uko mitaani bangi ina majina mengi na watumiaji wake wameipa majina kama: dope, nyasi, majani, m… Read More
  • ATHARI ZA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYAMADHARA YA DAWA ZA KULEVYA:Matumizi na biashara ya dawa za kulevya yameendelea kusababisha madhara makubwa mbalimbali nchini yakiwemo ya kiafya, kijamii, kiuchumi, kimazingira, kisiasa na kiusalama.KIAFYA:Dawa za kulevya zime… Read More
  • JIKINGE AU JITIBU ‘PRESHA YA KUSHUKA ’ KWA CHAKULAPresha ya kushuka au shinikizo la chini la damu (hypotension) hali hii inatokea pale msukumo wa damu unapakua mdogo na dhaifu, halo ambayo husababisha viungo muhimu katika mwili (major organs) kushindwa kupokea kiasi cha damu… Read More
  • VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGOBILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furah… Read More

1 comments:

  1. Kweli uvutaji wa bangi ni hatari sana kwa afya wavutaji

    JibuFuta