Ijumaa, 14 Aprili 2017

KILIMO CHA BAMIA


 BAMIA
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.

Urefu wa mmea huwa kati ya meta moja na mbili. Matunda yake hufikia urefu wa sentimeta 10 hadi 20, na huchumwa kabla hayajakomaa sana na hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Majani yake huchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

Ustawishaji: Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

Kupanda: Kwa kawaida mbega za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.

Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini. Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondo ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka. Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

Magonjwa: Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

Related Posts:

  • KILIMO BORA CHA TANGAWIZITangawizi ni moja kati ya aina za mazao ya viungo ambayo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Zao hili kwa lugha ya kigeni linafahamika kama Zingiber officinale.UDONGO NA KUSTAWIZao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya… Read More
  • FAHAMU KILIMO BORA CHA MIHOGO CHENYE TIJAZao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia … Read More
  • Kilimo Bora Cha Pilipili HohoJina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha.Kilimo hiki kinaende… Read More
  • MAAJABU YA MAFENESI ( ARTOCARPUS HETEROPHYLLUS LAM)MAFENESI au Jackfruits kwa lugha ya kiingereza na majina mengine Langka na Nangka ni matamu kwa ladha yake. Lakini pia yana umuhimu katika mwili wa binadamu.Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yak… Read More
  • KILIMO CHA MATANGOni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°CUdongo Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha majiMaandalizi ya shamba Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe … Read More

0 comments:

Chapisha Maoni