• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ufugaji. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ufugaji. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 13 Mei 2017

Dume Mzuri Kwa Uzalishaji Wa Ng’ombe Wa Maziwa


http://ufugajimakini.blogspot.com/

Tunaangalia uchaguzi wa dume mzuri kwa uzalishaji wa ng’ombe wa maziwa, pamoja na aina ya malisho ambayo mfugaji anaweza kuyatumia kuweza kukabiliana na changamoto ya malisho kwa ng’ombe.
Wafugaji wengi wamekuwa wakipata ng’ombe wanaozalisha kidogo na kwa kiwango cha chini kutokana na kuangalia ukubwa wa gharama ya mbegu wakidhania kuwa ndiyo upatikanaji wa ng’ombe bora. Vinasaba husaidia kwa kiwango kikubwa katika kupata ng’ombe mzuri wa maziwa.



http://ufugajimakini.blogspot.com/

Kuwepo kwa ongezeko la uzalishaji wa maziwa hutegemeana na vitu viwili ambavyo ni kuboresha mifugo kwa kufanya uchaguzi sahihi wa kizazi pamoja na usimamizi mzuri unaojumuisha lishe kamili, malazi mazuri, upatikanaji wa maji,kuwa karibu na wanyama pamoja na utoaji wa kinga na tiba dhidi ya magonjwa.



Vinasaba pamoja na usimamizi mzuri ni vitu viwili vinavyotegemeana. Bila kuwa na uzao mzuri, uzalishaji wa wanyama pamoja na usimamizi utakuwa wa hali ya chini sana, na bila usimamizi mzuri wanyama bora hawawezi kuonesha ubora wao katika uzalishaji.



Uzao mzuri humpa nafasi kubwa mfugaji kutambua sifa na uzalishaji utakaopatikana katika uzao ujao. Endapo mfugaji atafanya uchaguzi mbaya basi ni hakika atakuwa na uzalishaji hafifu wa maziwa, kuzorota kwa afya ya mnyama pamoja na maisha mafupi.



Muda wa kufanya tafiti



Wafugaji wengi wamekuwa wakifikiria mbegu pale tu ng’ombe anapokuwa tayari anahitaji kupandwa na matokeo yake ni kuwa, kutokana na haraka ya kutaka kumhudumia ng’ombe huyo, basi mfugaji atakuwa tayari kuchukua mbegu yoyote ile atakoyopatiwa na wataalamu. Kwa mantiki hiyo, hakuna muda mfugaji atatumia kuchunguza aina ya dume aliyetumika kupatikana kwa mbegu hiyo na badala yake, gharama hutumika kwa kiasi kikubwa kuonesha uwezo wa dume huyo.



Wafugaji wengi hufikiri kuwa kitendo cha mbegu kuuzwa kwa gharama kubwa ni moja ya njia ya kutambua ubora wa dume. Wauzaji wengi wamekuwa wakitumia njia hii kuwadanganya na kuwarubuni wafugaji.



Ni muhimu sana kwa mfugaji anaelenga kuzalisha maziwa kusoma na kuelewa taarifa zote muhimu zilizotolewa kuhusu aina ya dume husika. Ili kufanikiwa katika uzalishaji wa maziwa, ni muhimu kwa mfugaji kuwa makini na kulichukulia kwa uzito suala la uchaguzi wa dume na kuelewa nini kinahitajika bila kubahatisha. Mfugaji ni lazima atambue kuwa, dume huchangia asilimia 50 ya kinasaba katika uzao wake hivyo ni muhimu sana kujua sifa za dume unayemchukua kwa ajili ya uzalishaji. Pia ubora wa maziwa huchangiwa kwa kiasi kikubwa na aina ya dume aliyetumika. Dume wa maziwa hutambulika kwa kuangalia kiwango cha maziwa yanayozalishwa na ng’ombe aliyepandwa na dume huyo na mtamba aliyezaliwa na ng’ombe huyo ambapo dume huyo husambaza sifa ya maziwa kutoka kwa ng’ombe huyo hadi kwa mtamba.



Elewa maelekezo yaliyopo kwenye kabrasha la mbegu



Kielelezo cha vinasaba hutumika kupima uwezo wa mnyama kusambaza vinasaba vyake kwenda kwa uzao ujao. Katalogi huwa na taarifa muhimu ambazo zitamsaidia mfugaji kufanya uchaguzi mzuri wa dume ili kuwa na uhakika wa kuendeleza kizazi baada ya kingine.


Jumatano, 19 Aprili 2017

AINA ZA NGOMBE WA MAZIWA


Ndugu msomaji leo nitakuletea kitu kipya na chenya manufaa sana ukikizingatia,hizi ni aina ya ng'ombe wa maziwa waliopo duniani

MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE UCHAGUZI WA NG'OMBE MZURI WA MAZIWA

Umbo : siku zote ngo'mbe wa maziwa anatakiwa awe na umbola pembe tatu, humpless pia awe na miguu imara pamoja na tumbo kubwa kwa sababu ng'ombe mwenye tumbo kubwa anaweza kula sana na kutunza chakula kingi.na chakula kingine kinabadilishwa na kua maziwa.hivyo ng'ombe mwenye tumbo kubwa anauwezo wa kutoa maziwa mengi sana.

Kiwele na chuchu: siku zote ng'ombe mzuri wa maziwa anakiwele kizuri kimeshika vizuri kwenye mwili na kiwele kizuri hua kinabonyea kama spongy.na pia kiwele na chuchu vinatakiwa kua kubwa.

Rangi ya mwili : sikuzote ng'ombe mzuri wa maziwa anarangi moja au mbili tu kwenye mwili wake e.g brown, red white and black.

Asili : siku zote ng'ombe mzuri wa maziwa anatokea katika maeneo yenye hali ya hewa ya kati e.g Holland, Switzerland, Scotland and other part of Europe and Asia.

AINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA

Kuna makundi mawili ya ng'ombe kuna wa nyama pamoja na wamaziwa. na kuna aina nyingine pia ni wazuri kwa nyama pamoja na wamaziwa mfano mpwapwa na sahiwal.

hizi hapa na aina za ng'ombe wa maziwa

  • Holstein Friesian



  • Brown swiss



  • Ayrshire



  • Guernsey



  • Jersey



  • Mpwapwa



  • Sahiwal



  • Red pollAINA ZA NG'OMBE WA MAZIWA NA SIFA ZAKE

    1.HOLSTEIN FRIESIAN

    Hii ni aina ya ng'ombe wa maziwa ambayo ni kubwa kuliko aina zote

    SIFA

    • Asili yake ni Holland



    • wanamabaka meupe na meusi



    • maziwa yao yana mafuta kiasi cha 3.5%



    • wanatoa maziwa mengi 6000 liters kwa kila msimu wa kukamua



    • watoto wake wanazaliwa wakiwa na 40 kg na zaidi.



    • jike anauzito wa 400-600kg na dume 600-1000kgs



    1. BROWN SWISS


    Hii ni kati ya aina za zaman sana, ili gunduliwa katika milima ya Switzerland?

    SIFA

    • Wame gunduliwa Switzerland



    • hii ni aina nzito inayo fuata baada Friesian



    • wanalangi ya brown inayo koza



    • niwapole



    • uzito wa jike 450-550kg na dume 600-900kgs



    1. AYSHIRE


    Hii ni aina kubwa inayo fata baada yaFriesian na brown Swiss

    SIFA

    Niwakubwa zaidi ya jersey na Guernsey

    wanarangi nyekundu kuelekea mahogany mchanganyiko na nyeupe

    asili yao ni South west Scotland

    maziwa yao yanamafuta 4%

    wanachuchu na kiwele kizuri sana

    1. Guernsey


    SIFA

    wanatoa maziwa yenye langi kama ya dhahabu

    wanarangi nyeupe na nyekundu

    maziwa yao yanamafuta 4.5%

    wanatoa maziwa 4200litres kwa msimu mmoja wa kukamua

    uzito wa jike 450-500kgs na dume 600-700kgs

    1. Jersey


    hii ndo aina ndogo kuzudi zote

    SIFA

    • asili yao ni visiwani kati ya UK na France



    • maziwa yao yanamafuta kuzidi wote 5%



    • wanarangi ya blackish brown



    • uzito wa jike 400-450kg dumeto 500-600kgs.


    asante mpenzi msomaji endelea kua na mimi upate kujifunza mengi kwa tasinia ya kilimo pamoja na ufugaj

Ijumaa, 7 Aprili 2017

Ufugaji Bora wa Bata Mzinga


Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi. Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.


Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.


Chakula

Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita. Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa. Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.


Mahitaji



  • Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa)

  • Karanga 5kg

  • Dagaa 5kg

  • Mashudu 10kg

  • Chokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo)


Namna ya kutengeneza chakula
Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa. Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.


Uhifadhi
Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.


Kutaga

Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.


Kuhatamia

Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.


Utunzaji wa vifaranga

Baada ya vifaranga kuanguliwa, watenge na mama yao kwa kuwaweka kwenye banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya kandili au ya umeme endapo upo kwenye sehemu unakopatikana.


Banda

Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi. 


Maji

Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.


Magonjwa

Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.


Chanjo

Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano – ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.

Jumatano, 29 Machi 2017

UFUGAJI WA SAMAKI


Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).


Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.