• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Jumatano, 19 Aprili 2017

Matumizi ya Mbolea


Matumizi ya rutuba kwenye udongo

  • } Mimea huchukua /huondoa virutubisho kutoka kwenye udongo kupitia kwenye mizizi.

  • } Virutubisho vinavyotumika na nafaka kama (ngano, mahindi, mpunga, n.k) inageuzwa kuwa punje na sehemu kwenye masalia ya mimea.

  • } Kwa upande wa mahindi ,kwa kila kilogramu 1000 ya mazao yanayozalishwa ,Kilogramu 35 za virutubisho zinakuwepo kwenye mazao na kilogramu 37 kwenye masalia  ya mimea.Jumla ya kilogramu 72 za virutubisho zinakuwa zimetoweka.

  • } Iwapo kwenye hekta moja umevuna tani 4 =kilogramu 4000, kiasi cha kilogramu 288 ya virutubisho itakuwa imeondolewa kutoka kwenye udongo.

  • } Kama hivi virutubisho havitarudishwa, rutuba ya udongo itapungua .Kwa miaka kadha wa kadha, mavuno kutoka kwenye udongo wa aina hiyo inashuka.

  • } Kwa udongo kubaki na rutuba, ni vizuri kurudisha virutubisho vilivyo potea wakati wa mavuno ya mazao.


Kutoka: IFDC: Estimated removal of nutrients from the soil by Grains (kg nutrients/ Mt grain harvested)































MimeaNitrojeni

(N)
Fosforasi

(P2O5)
Potasiamu

(K2O)
Jumla
Mahindi1810735
Ngano208533
Mpunga146424

Kutoka: IFDC: Estimated removal of nutrients from the soil by          Residue (kg nutrients/ Mt straw harvested)































MimeaNitrojeni

(N)
Fosforasi

(P2O5)
Potasiamu

(K2O)
Jumla
Mahindi1062137
Ngano632231
Mpunga922435

Virutubisho ni nini?

  • } Mimea inahitaji virutubisho kumi na sita ili kukua na kutoa maua na mazao mazuri.

  • } Virutubisho hutumika kama lishe ya mimea.

  • } Virutubisho vitatu hutoka hewani mambavyo ni: kaboni, oxijeni na hydrojeni.—Ikichangia asilimia 93 ya mahitaji ya mmea.

  • } Wakati virutubisho vitatu hutokana na hewa na maji .

  • } vingine kumi na tatu hupatikani kupitia udongoni.Hupatikana kupitia mizizi na kutumika na mimea.


Madaraja ya virutubisho vya mimea

  • } Kwa kuzingatia kazi zake na kiwango kinachohitajika na mimea kwa ukuaji kumetokea madaraja yafuatayo:



  1. Virutubisho vya msingi au vinavyohitajika kwa wingi



  • } Nitrojeni (N), Fosforasi (P), Na potasiamu (K) ndivyo vinahitajika mno na mimea kwa ukuaji na kwa kiwango kikubwa.



  1. Virutubisho vinavyo hitajika kwa kiasi



  • } Kalsiamu (Ca), salfa (S), and magnesiamu (Mg) huhitajika kwa kiasi kidogo na mimea lakini vinaumuhimu mkubwa.



  1. Virutubisho vinavyo hitajika kwa kiwango kidogo



  • } Virutubisho saba vilivyobaki ambavyo ni: Chuma (Fe), Kopa (Cu), zinki (Zn), boron (B), manganese (Mn), clorini (Cl), and molybdenum (Mo) huhitajika kwa kiwango kidogo sana.


Dalili kutokana na ukosekanaji wa vitutubisho Dalili kutokana na ukosekanaji wa vitutubisho

Virutubisho vya msingi

  • } Nitrogen (N), phosphorus (P), and potassium (K) ni vya aina tatu.


Kutokana na makubaliano ya vigezo vilivyowekwa na viwanda vya mbolea, virutubisho vya muhimu /msingi vimekubalika kama; N (nitrogen), P2O5 (or phosphorus pentoxide for phosphorus), and K2O (or potassium oxide for potassium

  1. Nitrogen

  2. Nitrojeni ndio kirutubisho cha muhimu kwa aina kubwa ya udongo unaonjesha mapungufu.

  3. Ijapokuwa Nitrojeni inahitajika katika ukuaji wa awali wa mimea ,inahitajika kwa kiwango kikubwa wiki ya 3-4 kutoka zao kuota haswa kwa mazao ya nafaka kama ngano,mahindi ,mpunga n.k.

  4. Nyongeza huwekwa baadae wakati mimea inapacha ,kutoa maua au karibu na kukomaa.

  5. Kwa hiyo Nitrojeni huwekwa kama mara 2-3 kwenye mimea


Dalili za mapungufu ya  Nitrojeni

  • } Kama nitrojeni imekosekane kwenye udongo:

  • } Ukuaji wa mmea huwa taratibu.

  • } Mmea hudumaa na majani kuwa ya njano.

  • } Mmea hukomaa haraka kupunguza mavuno.



  • } Upungufu wa  Nitrojeni

  • } Mapungufu ya nitrojeni hupatikana karibu kila eneo lakini zaidi kwenye udongo wa kichanga, udongo wenye kiwango kidogo cha mboji, au udongo uliolimwa mfululizo kwa miaka mingi.

  • } Aina ya mbolea inayotumika sana kusambaza nitrojeni ni mbolea ya Urea,SA,CAN



































MboleaVirutubisho %

N:P:K
Hutumika haswa
Urea46:0:0Kukuzia
Calcium Ammonium Nitrate(CAN)27:0:0Kukuzia
Sulphate of Ammonia(SA)21:0:0Kukuzia
Di -ammonia Phosphate (DAP)18:46:0Kukuzia
N:P:K17:17:17,20:10:10Kukuzia


  1. Fosforasi



  • } Fosforasi hupitia kwa mmea kwa kutumia mbolea za fosfeti,mara nyingi hutumika kupandia.

  • } Fosfati ni muhimu sana kipindi cha awali cha ukuaji wa mmea  kwa kuuwezesha mmea kuwa na mizizi mingi na kuwa na nguvu ya kuushikilia mmea kwenye udongo.

  • } Mizizi yenye afya huufanya mmea kupata vitutubisho kwenye udongo.


Dalili za mapungufu ya fosforasi

  • } Upungufu wa Fosforasi Huonekana haswa kwenye udongo wenye tindikali au ulio na kalsiuamu /chokaa kwa wingi.

  • } Mapungufu ya fosforasi kwenye udongo huufanya mmea kuwa :

  • } Dhaifu kutengeneza mizizi.

  • } Kuanguka kwa mmea.

  • } Kudumaa kwa mmea na mavuno kidogo.

  • } Mfano wa mbolea zenye Fosforasi ni: SSP (0-16-0),TSP (0-46-0),DAP (18-46-0)



  1. Potasiamu



  • } Potasiamu ni aina ya tatu ya kirutubisho cha msingi kinachohitajika na mimea.,barafu ,wadudu na magonjwa na kusaidia usafirishaji wa virutubisho vingine kuanzia kwenye mizizi hadi sehemu nyingine ya mimea.

  • } Inasaidia kujaza punje,mbegu.

  • } Mbolea zote zinazosambaza Potasiamu hutumika kupandia ila kwenye udongo wa kichanga inashauriwa kuwekwa mara mbili wakati wa kukuzia.


Dalili za mapungufu ya potasiamu

  • } Majani huonjesha dalili ya kama kuungua kwenye njia ya jani na kuendelea.

  • } Kwa lugha ya kitaalamu huitwa “chlorosis.”

  • } Mimea inakuwa dhaifu kwa mashambulizi ya magonjwa.

  • } Salfa inahusika kwenye protini ya mmea ,husaidia vimengényo na vitamini vinavyohitajika kwenye kutengeneza ukijani unaosaidia kuakisi mwanga wa jua


.

  • } Sulfur inapatikana kwenye vitu vingi Kama vile gypsum na mbolea kama ammonium sulfate, SSP and TSP.


Matumizi ya mbolea Asilia/Mboji

  • } Mboji ni urutubishaji wa asili ambao hujirudia wenyewe kwa mtindo wa kuoza. Utengenezaji wa  mboji ni njia ya kurudisha rutuba ya asili kwenye udongo kwa njia ya kuozesha vitu.

  • } Matokeo yake ya mwisho ni kutoa mbolea asili ambayo ni rahisi kutengeneza, na ambayo ina virutubisho vingi bila gharama

  • } Mboji huwa ni faida kutokana na uozaji wa asili ambao hutokea kwenye vitu vyote vyenye uhai.

  • } Vitu vyenye uhai ni kama vile majani, miti na mabaki ya vyakula.wakati wa uozaji vitu hivi hugeuka na kuwa rutuba inayorudia kwenye udongo

  • } Udongo hupoteza virutubisho baada ya kutumika sana .

  • } Matumizi ya mbolea za asili nayo ni mazuri katika kuendeleza udongo kwa ajili ya ukulima.

  • } Pia mbolea za asili/mboji husaidia kuzuia mmomonyoko wa ardhi

  • } Inaruhusu mmea kupata rutuba kwa urahisi kutoka kwenye udongo.

  • } Pia hufanya mmea usiwe dhaifu kwahiyo huzuia wadudu waharibifu kushambulia mmea.

  • } Mboji hutoa virutubisho kwa muda mrefu kwasababu ya uendeleaji wa kuoza polepole.

  • } Madini yaliyopo katika mboji husaidia kuyeyusha madini mengine yaliyo kwenye udongo,

  • } Hufanya madini yenye rutuba yapatikane zaidi kwa mimea. Madini hayo huimarisha sehemu laini za mizizi na hivyo kuipa mizizi uimara wa kuweza kupata maji na virutubisho kwa njia ya mizizi


Hitimisho

  • } Mbolea ni kitu muhimu sana katika udongo kwa sababu mazao huitaji virutubisho katika udongo na baada ya udongo kutumika kwa muda mrefu , virutubisho hupotea.

  • } Kuvirudisha virutubisho, mbolea inahitajika inaweza ikawa ya chumvichumvi au ya asili hii hutegemea na udongo uliopo katika sehemu hiyo.

  • } Kila sehemu ina udongo wa aina yake na unahitaji virutubisho vya aina yake kwa wingi au kiwango kidogo.

  • } Kwa hiyo uwekaji wa mbolea katika udongo lazima utumie utaalamu ambao mkulima amepata kutoka kwa wataalamu wa kilimo au uzoefu.

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO


BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.
Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.

Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:

MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.

MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.

NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.

BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.

KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

Ijumaa, 14 Aprili 2017

KILIMO CHA BAMIA


 BAMIA
Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.

Urefu wa mmea huwa kati ya meta moja na mbili. Matunda yake hufikia urefu wa sentimeta 10 hadi 20, na huchumwa kabla hayajakomaa sana na hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Majani yake huchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

Ustawishaji: Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

Kupanda: Kwa kawaida mbega za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.

Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini. Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondo ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka. Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

Magonjwa: Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

Alhamisi, 13 Aprili 2017

ATHARI ZA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA


MADHARA YA DAWA ZA KULEVYA:
Matumizi na biashara ya dawa za kulevya yameendelea kusababisha madhara makubwa mbalimbali nchini yakiwemo ya kiafya, kijamii, kiuchumi, kimazingira, kisiasa na kiusalama.

KIAFYA:
Dawa za kulevya zimeendelea kuleta madhara makubwa kiafya yakiwemo magonjwa ya akili, utegemezi wa dawa za kulevya, magonjwa ya mapafu, moyo, ini na figo. Aidha, matumizi ya dawa za kulevya yaliendelea kusababisha vifo vya ghafl a hasa miongoni mwa wajidunga kutokana kuzidisha dozi. Pia, matumizi ya dawa hizo yameendelea kuchangia kuenea kwa maambukizi ya VVU, kifua kikuu na virusi vya homa ya ini aina ya B na C. Watumiaji wengi wameendelea kukabiliwa na magonjwa ya meno na ngozi yakiwemo majipu, vidonda na ukurutu. Dawa za kulevya zimeendelea kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume, ugumba, utasa na kuzaliwa kwa watoto wenye ulemavu, njiti na wenye matatizo ya ukuaji wa kiakili na kimwili. Jedwali Na.8 linaonesha viwango vya maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa watumiaji waliojitokeza kupata matibabu kwenye hospitali za Muhimbili.

KIUCHUMI:
Matumizi ya dawa za kulevya huongeza mzigo kwa taifa kwa kuwa hupunguza nguvu kazi na husababisha uharibifu wa mali. Vilevile, gharama za udhibiti zikiwemo utoaji wa elimu kwa umma, uteketezaji wa mashamba ya bangi, uendeshaji wa kesi, kuwatunza wafungwa magerezani na kuwatibu watumiaji huongeza mzigo kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Biashara ya dawa za kulevya husababisha mfumuko wa bei unaotokana na fedha za biashara hiyo kuingizwa kwenye mfumo halali. Aidha, matumizi ya dawa zakulevya husababisha utoro mashuleni au kazini, kusitisha masomo au kufukuzwa kazi. Kwa ujumla, matumizi na biashara ya dawa za kulevya vimeendelea kuchangia kuongeza umaskini nchini.

KIJAMII:
Dawa za kulevya zimeendelea kusababisha mmomonyoko wa maadili katika jamii. Utumiaji na biashara ya dawa za kulevya mitaani husababisha tabia hiyo kuzoeleka na hivyo kuwavutia watu wengine hasa watoto kujiingiza kwenye tatizo hilo na kuchangia kuharibika kwa kizazi kijacho.Aidha, matumizi ya dawa ya hizo huchangia migogoro ya kifamilia katika jamii jambo linaloweza kuzisambaratisha kabisa. Wazazi ambao hutumia dawa za kulevya, huonesha mfano mbaya kwa watoto wao na jamii kwa ujumla. Pia, kumekuwepo na ajali zilizosababishwa na uendeshaji wa magari na mashine huku waendesha vyombo hivyo wakiwa wametumia dawa za kulevya. Ajali hizo mara kwa mara zimekuwa zikisababisha ulemavu na vifo vingi. Wajidunga hutupa ovyo mabomba ambayo huweza kusababisha majeraha kwa wapita njia au maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Watumiaji wamekuwa wakijihusisha na tabia na vitendo viovu vikiwemo wizi, uporaji, biashara ya ngono na ubakaji. Jamii imekuwa ikiamini kuwa matumizi ya dawa za kulevya ni jambo la kujitakia, hivyo kuwanyanyapaa na kuwabagua watumiaji. Vitendo na muonekano wao huwafanya wasikubalike katika jamii jambo linalosababisha kuendeleza vitendo vyao vya uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya. Halikadhalika, kosa la kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya huambatana na adhabu kali ikiwemo kifungo cha maisha jambo ambalo linawatenga wahusika na familia zao pamoja na jamii. Biashara ya dawa za kulevya huhusisha rushwa kubwa ambayo huathiri utoaji haki kwa wananchi na utawala bora. Wafanyabishara wa dawa za kulevya hutumia sehemu ya faida wanayopata kusaidia jamii ambayo huwaonea aibu kuwachukulia hatua pindi wanapojihusisha na vitendo viovu.

Wafanyabiashara hujitumbukiza kwenye vitendo vya kihalifu kama utekaji nyara, ugaidi, mauaji ya kikatili, vita vya wenyewe kwa wenyewe na ujambazi, hivyo kusababisha uvunjifu wa amani. Vilevile, wafanyabiashara wa dawa za kulevya huweza kuwarubuni watendaji wa vyombo vya udhibiti wa dawa za kulevya kuvujisha siri hivyo kuhatarisha maisha ya watendaji na raia wema.

KISIASA:
Wafanyabiashara wa dawa za kulevya huweza kuwashawishi wapiga kura kwa kutumia rushwa kuwachagua viongozi watakaosimamia maslahi yao pindi watakapokuwa madarakani. Biashara ya dawa za kulevya huweza kuchochea machafuko ya kisiasa na kuweza kupindua serikali iliyopo madarakani. Halikadhalika, nchi inayojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya huharibu taswira ya nchikimataifa na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo raia wake kutoaminika na kupata usumbufu mkubwa wanapokuwa kwenye nchi nyingine.

KIMAZINGIRA:
Kilimo cha bangi kinachofanyika kwenye vyanzo vya maji na kwenye ardhi oevu husababisha kukauka kwa mito na kuleta ukame. Pia, ukataji miti ovyo na uchomaji moto wa misitu kwa ajili ya kuandaa mashamba ya bangi husababisha mmomonyoko wa udongo.

NB:
Kila ifikapo tarehe 26 mwezi wa 6 kila mwaka,hua ni siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya duniani.

Jumatano, 12 Aprili 2017

MADHARA YA BANGI


Bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Uko mitaani bangi ina majina mengi na watumiaji wake wameipa majina kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga.

Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa
Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish.

Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe
(hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake.Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.

Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu,maua, na mche na huwa na rangi ya kijani,kijivu au brauni na bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika sehemu nyingi duniani.

Bangi hutumika kwa kuvuta moshi kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake. Ni mara chache huchanganywa katika chakula, kuliwa kama mboga au kutengeneza kinywaji. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na watumiaji kama “blunt”

Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo katika uhalisia (ndoto za mchana/maruweruwe).Matokeo haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC kilichovutwa na ukali wake.

Mara nyingi wavutaji wa bangi huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.

Matatizo ya ubongo yanayopelekea kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.

Jumamosi, 8 Aprili 2017

Vyakula bora kwa afya ya mama na mtoto


Lishe ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto – hili si jambo geni sana. Lishe bora ni lazima kwa watoto wadogo sababu wanatakiwa kukua vizuri – kimwili na kiakili.

Je lishe bora ni ipi?

Lishe bora ni chakula chenye virutubisho vyote muhimu kwa kiasi na uwiano sahihi ili kuuwezesha mwili wa mtoto kupata siha nzuri (afya bora). Wataalamu wanachambua zaidi kwa kusema kuwa lishe bora ina virutubisho aina sita, ambayo ni: Wanga, Protein, Mafuta, Vitamin, Madini na Maji.

Je vyakula gani ni bora ?

Lishe bora inatakiwa kuwa na mboga za majani, matunda, protini, wanga na madini ya kutosha. Hizi zinapatikana kwenye vyakula aina tofauti, na kuna vyakula vingine vina virutubisho vingi kwa pamoja.

Mfano wa vyakula vyenye lishe bora kwa kiwango kinachofaa ni kama mboga za majani, mafunda, nafaka asilia, vyakula vya protini (mayai, maharage, nyama n.k) na vyakula vyenye mafuta yasiyohifadhiwa mwilini.
Watoto wanagawanywa kwenye makundi ya aina mbili : Kuzaliwa hadi miezi 6 na kuanzia miezi 6 na kuendelea. Haya makundi ni muhimu sababu watoto waliopo kwenye makundi haya wanatofautiana aina za vyakula wanavyokula. Ni muhimu kuzingatia hili sababu huu ndio muda muhimu zaidi katika ukuaji wa mtoto.

Lishe ya mtoto mchanga hadi miezi 6


Inashauriwa kuwa mtoto mchanga – tangu anazaliwa hadi afikapo miezi 6 – asipewe kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama, hii ikiwa inamaanisha hata maji ya kunywa. Maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu (pamoja na maji) vinavyohitajika kwenye ukuaji mzuri wa mtoto na kumpa kinga ya magonjwa mbalimbali.

Photo by Google

Lishe ya mtoto kuanzia miezi 6


Mtoto akishafika umri wa miezi 6, anaweza kuanza kula vyakula mbali mbali. Inashauriwa mtoto aanze kupewa vyakula mbali mbali kidogo kidogo ili apate kuzoea. Vyakula hivi lazima view vimepondwa, au viwe kwenye mfumo wa uji au maji sababu mtoto anakuwa hana meno yaliyokomaa au wengine wanakuwa hawajaanza kabisa kuota meno.

Lishe ya Mama


Ukizungumzia mtoto hutoweza kuacha kuzungumzia mama. Mama ndiyo chanzo kikubwa cha chakula kwa mtoto tangu anazaliwa hadi anakuwa huru kula chakula cha kawaida. Kwa mwanamke mwenye umri wa kubeba ujauzito au mwenye ujauzito, ni muhimu kula vizuri ili kujenga afya ambayo ndio chanzo kikubwa cha virutubisho kwa mtoto tumboni na baada ya kuzaliwa. Ili kuwa na siha nzuri, vyakula vyote vinatakiwa kuwa na uwiano mzuri wa virutubisho.

Inatakiwa kuzingatiwa kuwa, vyakula vya mtoto viwe vya kuongezea lishe, lakini ni vizuri mtoto akiendelea kunyonya maziwa ya mama hadi atakapofikisha miezi 24. Maziwa ya mama ni muhimu katika kumfanya mtoto akue vizuri, hasa katika miezi 24 ya mwanzo. Inashauriwa kuwa, kama hakuna kikwazo – mfano: ugonjwa wa maambukizi unaoweza kumdhuru mtoto – ni vizuri mama amnyonyeshe mtoto kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita (6).

Faida kubwa ya kunyonyesha ni kusaidia ubongo wa mtoto kukua vizuri zaidi sababu maziwa ya mama yanatoa virutubisho kwa wingi kuliko vyakula atakavyokula yeye moja kwa moja. Hii ni kwa sababu, tumbo la mtoot linakuwa halijazoea kusaga vyakula tofauti, hivyo maziwa ni chakula kinacholeta virutubisho vinavyotumika moja kwa moja mwilini.

Umuhimu wa lishe bora


Kama ilivyoelezwa mwanzo, lishe bora ni muhimu. Zifuatazo ni baadhi ya faida apatazo mtoto anayepata lishe bora:

  • Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini na kuufanya mwili kupambana kirahisi na magonjwa kama utapiamlo (kwashiorkor) na kiriba tumbo

  • Kujenga siha nzuri (afya bora)

  • Kuleta furaha na Amani

  • Kusaidia ukuaji wa mwili na akili

  • Kuleta nguvu na kusaidia mwili kufanya kazi vizuri


Madhara ya lishe duni


Kama mtoto akiwa na lishe duni, haya yatakuwa madhara yake:

  • Kupata magonjwa mara kwa mara sababu anakosa kinga madhubuti dhidi ya magonjwa

  • Kudumaa kukua mwili na akili

  • Uwezekano mkubwa wa kupata ulemavu sababu mifupa inakuwa laini na haiwezi kustahimili uzito wa mwili.

  • Upungufu wa damu hivyo kudhoofisha afya ya mtoto

  • Kupata utapiamlo (Kwashiorkor)

  • Kupoteza maisha katika umri mdogo

Ijumaa, 7 Aprili 2017

Ufugaji Bora wa Bata Mzinga


Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi. Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.


Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.


Chakula

Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita. Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa. Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.


Mahitaji



  • Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa)

  • Karanga 5kg

  • Dagaa 5kg

  • Mashudu 10kg

  • Chokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo)


Namna ya kutengeneza chakula
Twanga au saga pamoja kiasi cha kulainika kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa. Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.


Uhifadhi
Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.


Kutaga

Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.


Kuhatamia

Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.


Utunzaji wa vifaranga

Baada ya vifaranga kuanguliwa, watenge na mama yao kwa kuwaweka kwenye banda safi lisilopitisha baridi. Unaweza kuwawekea taa ya kandili au ya umeme endapo upo kwenye sehemu unakopatikana.


Banda

Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi. 


Maji

Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.


Magonjwa

Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.


Chanjo

Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano – ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.