• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Jumatatu, 13 Septemba 2021

Fahamu sifa, faida na changamoto za ufugaji kuku wa asili






Kuku wa asili ni aina ya kuku ambao wamekuwepo nchini kwa muda wa miaka mingi na damu au koo zao hazikuchanganywa na aina yeyote ya kuku wa kienyeji. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbalimbali.

Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa asili nchini Tanzania hufanywa na wafugaji wadogo wadogo wanaoishi kandokando ya miji na wale wanaoishi hasa vijijini.

Kuku hawa wa asili hufugwa kwa mtindo huria yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa na kuachiwa huru asubuhi ili wajitafutie chakula.

Kuku wa asili hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai; Kwa mfano kuku mmoja wa asili hutaga kiasi cha mayai 40 hadi 60 kwa mwaka badala ya 100 hadi 150 iwapo atatunzwa vizuri.

Aidha, uzito wa kuku hai ni chini sana, wastani wa kilo 1.0 hadi 1.5 kati ya umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8 hadi 2.5 iwapo anapata matunzo vizuri.

Sifa za kuku wa asili

  • Kuku wa asili ni wastahimilivu wa magonjwa, lakini ni muhimu wakikingwa na baadhi ya magonjwa ya kuku kama vile mdondo, ndui ya kuku na ikiwezekana wapewe kwa kuendeleza.
  • Kuku wa asili wana uwezo wa kujitafutia chakula lakini ni muhimu kuwapa chakula bora na cha ziada.
  • Kuku hawa wana uwezo wa kuhatamia mayai, kutotoa, kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu (ukame, baridi).
  • Nyama na mayai ya kuku wa asili vina ladha nzuri sana kuliko kuku wa kisasa.
  • Kwa kiasi fulani kuku wa asili wana uwezo wa kujilinda na maadui kama vile mwewe.
  • Pamoja na sifa hizi ni muhimu sana kuku hawa wakapewa matunzo mazuri, wawekwe kwenye mabanda mazuri na imara, na pia wapewe maji na chakula cha kutosha.

Faida za ufugaji wa kuku wa asili

  • Chakula; Kuku wa asili wanatupatia nyama na mayai ambayo hutumika kama chakula muhimu cha wanadamu, chenye protini.
  • Chanzo cha kipato; Mkulima huweza kujipatia kipato kwa kuuza kuku au kuuza mayai.
  • Chanzo cha ajira; Ufugaji wa kuku ni mojawapo ya ajiira kwa jamii.
  • Kuku hutumika kwenye shughuli za ndoa kama vile kutoa mahari kwa baadhi ya makabila lakini pia ni kitoweo muhimu katika sherehe hizo.
  • Gharama nafuu katika kuanzisha na kuendesha mradi huu.
  • Kuku wa asili ni kitoweo rahisi na chepesi kwa wageni kuliko wanyama wakubwa kama ng’ombe au mbuzi na ni kitoweo kisichohitaji hifadhi kwani hutumika kwa mlo mmoja au miwili na kumalizika.
  • Kuku na mayai pamoja hutumika pia kwa tiba za asili.
  • Jogoo hutumika kama saa anapowika nyakati za alfajiri na katika majira mengine ya siku.
  • Kuku hutuhabarisha iwapo kiumbe kingine kigeni au cha hatari kimeingia kwa mlio wake maalumu wa kuashiria hatari.
  • Mbolea au kinyesi cha kuku kinaweza kutumika katika kurutubisha mashamba ya mazao na mabwawa ya samaki.
  • Kuku wa asili pia hutumika katika kuendeleza kizazi cha kuku nchini.
  • Soko la kuku wa asili lipo juu na la uhakika ukilinganisha na kuku wa kisasa kwani nyama na mayai yake hupendwa zaidi na walaji.
  • Manyoya ya kuku wa asili hutumika kama mapambo na pia huweza kutumika kutengenezea mito ya kulalia na kukalia.
  • Shughuli za utafiti zinaonyesha kuwa kuku wa asili wanatumika katika tafiti nyingi za baiolojia kama kutambua mambo ya lishe.
  • Shughuli za viwandani; Mayai ya kuku wa asili yenye mbegu ya jogoo hutumika katika kutengenezea dawa za chanjo.
  • Magamba ya mayai ya kuku wa asili yanweza kutumika katika kutengeneza vyakula vya wanyama.
  • Kiini cha njano cha mayai ya kuku wa asili hutumika kutengenezea mafuta ya kuoshea nywele.

Mapungufu ya kuku wa asili

Kuku wa asili hutaga mayai madogo wastani wa gramu 47 ambapo kuku wa kisasa hutaga yai la wastani wa gramu 55.

Aidha, kuku wa asili hutaga mayai machache wastani wa mayai 60 kwa mwaka ambapo kuku wa kisasa huweza kutaga hadi mayai 300 kwa mwaka.

Kuku wa asili hukua taratibu kutokana na lishe duni. Kutokana na hali hii kuku huchukua muda mrefu (miezi sita) kufikia uzito wa kuchinja (kilo 1 hadi 1.5). Na hali hii pia hufanya faida ya ufugaji wa kuku wa asili kuchukua muda mrefu kupatikana.

Nyama ya kuku wa asili ni ngumu (huchukua muda mrefu kuiva) ikilinganishwa na nyama ya kuku wa kisasa.

Changamoto katika ufugaji wa kuku wa asili

Ukosefu wa mabanda yenye ubora, wezi, wanyama na ndege wengine hushambulia kuku.

Magonjwa kama vile mdondo na  ndui huathiri ufugaji wa kuku.

Tabia ya miiko ya baadhi ya jamii au makabila hapa nchini ambayo huona ufugaji wa kuku kama ni kitu duni.

Upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa kama vile mdondo, ndui na homa ya matumbo hasa katika maeneo ya vijijini. 

Mifumo ya ufugaji wa kuku wa asili

Kuna mifumo mitatu ya ufugaji wa kuku wa asili inayotumika nchini Tanzania ambayo ni ufugaji huria, ufugaji nusu huria na ufugaji wa ndani na kila mfumo una faida na hasara zake.

Ni vyema mfugaji kujua mifumo yote na kisha kuchagua anaoona ni bora kulingana na mazingira yake. Hata hivyo katika kufanya uteuzi ni vyema kutilia maanani mfumo wenye faida zaidi na kuepuka mfumo wenye hasara nyingi.

Ufugaji huria

Katika mfumo huu kuku huachiwa kuanzia asubuhi wakitembea kujitafutia wenyewe chakula na maji na kufungiwa vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si mzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

Faida za ufugaji huria

Ufugaji huu ni wa gharama ndogo kwani gharama za kujenga uzio hazihitajiki.

Gharama za chakula hupungua kwani kuku huokota wadudu na kujilia baadhi ya majani.

Hasara za mfumo huria

  • Kuna uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheChe, mwewe na wanyama wengine, kuibiwa mitaani au kukanyagwa hata na magari.
  • Kuku hutaga popote na upotevu wa mayai huwa ni mkubwa.
  • Katika mfumo huu kunakuwako na usimamizi hafifu wa kundi la kuku na pia ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa.
  • Utagaji wa kuku unakuwa si mzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
  • Uwekaji wa kumbukumbu si mzuri na mara nyingi kumbukumbu si sahihi.
  • Si rahisi kugundua kuku wagonjwa na utoaji wa tiba na kinga ni mgumu lakini pia vifaranga wengi huweza kufa na hata wakati mwingine kupotea.

Namna ya kuboresha mfumo huu

Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine wowote kuwakinga na hali ya hewa inapokuwa si nzuri.

Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji lakini pia kuku waandaliwe viota maalumu kwa ajili ya kutagia.

Kuku 100 watumie eneo la ardhi a ekari moja ili kuwapa uwiano katika eneo.

Ufugaji nusu huria

Katika mfumo huu kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa wigo (uzio) na wigo huo hujengwa kwa mbele ambapo kuku hulala ndani ya banda nyakati za usiku na kushinda nje ya banda (ndani ya wigo)nyakati za mchana wakila chakula na kunywa maji humo.

Mfumo huu wa nusu huria ni ghali kiasi kuliko mfumo huria lakini huweza kumpatia mfugaji tija kubwa na kwa haraka sana.

Faida za mfumo huu

Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko sehemu inayotumika katika ufugaji huria na utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na ule wa huria.

Ni rahisi kutibu na kukinga maradhi ya milipuko kama mdondo na upotevu wa kuku na mayai ni mdogo ukilinganisha na mfumo huria na pia uwekaji wa kumbukumbu ni rahisi.

Hasara zake

Mfumo huu unahitaji gharama za banda na uzio na pia gharama za chakula zitakuwa kubwa kidogo ukilinganisha na ufugaji huria.

Matumizi ya muda mrefu ya eneo husika laweza kuwa na minyoo au vimelea vingine vyovyote vya magonjwa.

Uboreshaji wa mfumo huu

Fanya usafi wa eneo husika na banda kila siku na ikiwezekana pia kuwe na mzunguko wa kutumia eneo hilo.

Muhimu: Ili mfugaji aweze kupata tija na mafanikio katika ufugaji wa kuku wa asili anashauriwa atumie mfumo huu.

Ufugaji wa ndani

Katika mfumo huu, kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani huku wakipatiwa chakula, maji na kufanyiwa huduma nyingine muhimu wakiwa humo bandani kwa muda wote wa masha yao.

Kwa mfumo huu, kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa matandiko ya makapi ya mounga, takataka za mbao (randa), maganda ya karanga au majani makavu yaliyokatwakatwa.

Faida zake

  • Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia hivyo ni mzuri kwenye maeneo yenye uhakika wa ardhi.
  • Uangalizi wa kuku ni mzuri na rahisi na pia ni rahisi kuhakikisha ubora wa chakula.
  • Hakuna haja ya kufagia vinyesi vya kuku kila siku
  • Kuku wanakuwa wanakingwa na hali ya hewa na maadui wengine.
  • Ni rahisi kukinga na kutibu maradhi ya kuku lakini pia uwekaji wa kumbukumbu ni rahisi.
  • Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, vifaranga na mayai.

 

Hasara zake

  • Uwezekano wa kuku kudonoana na kula mayai ni mkubwa kama utunzaji utakuwa duni
  • Uwezekano wa kuku kuhatamia mayai bila mpangilio ni mkubwa
  • Ujenzi wa mabanda na ulishaji una gharama kubwa na mahitaji makubwa ya nguvu kazi.
  • Kuku watakosa mionzi ya jua ambayo ni muhimu sana kwa kuwapatia vitamin D.
  • Ni rahisi ugonjwa kuenea haraka unapoingia kwenye kundi.

Muhimu: Kutokana na uwezo mdogo wa uzalishaji kimaumbile, kuku wa asili hawataleta tija kwa mfugaji iwapo atatumia mfumo huu.

Uboreshaji wa mfumo huu

Hakikisha utumzaji mzuri wa matandiko na usafi wa banda ili kupunguza unyevunyevu na joto kali ndani ya bandi.

Kuku wawe na nafasi ya kutosha, mita mraba moja hutosha kuku kuanzia 5 hadi 8.

Maandalizi ya ufugaji wa kuku wa asili

Ili kuweza kufuga kuku wa asili kwa faida, ni vyema kufanya maandalizi ya awali yatakayokuwezesha kuzalisha kuku walio bora.

Maandalizi hayo yanajumuisha utayarishaji wa banda kulingana na idadi ya kuku utakaowafuga, uchaguzi wa kuku bora na uandaaji wa vifaa vya kulisha na kutagia pamoja na uwiano wa kuku ndani ya banda.

Banda bora

Ni muhimu kuwajengea kuku banda bora ili wapate kujikinga na mvua, baridi, wezi na wanyama. Banda la kuku linaweza likajengwa kando kando au nyuma ya nyumba ya kuishi .

Eneo la banda la kuku liwe ni eneo ambalo; Linafikika kwa urahisi, lisituamishe maji na lisiwe na mwelekeo wa upepo mkali.

Banda la kuku linaweza kujengwa kwa kutumia rasilimali za misitu zinazopatikana kwa urahisi kwenye eneo husika. Vifaa muhimu katika ujenzi wa banda ni pamoja na miti, nyasi, mabati, makuti, fito, udongo, mabanzi, saruji na vifaa vingine mbalimbali vya ujenzi.

Kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi

Mafanikio zaidi katika kuchagua kuku wa kuendeleza kizazi yatapatikana iwapo uchaguzi na uchambuzi wa kuku wanaozaliwa utafanywa mara kwa mara.

Sababu kubwa ya kufanya uchaguzi ni kupata kundi la kuku litakalofaa kwa sifa zote katika uzalishaji. Sifa hizo ni pamoja na kupevuka haraka, kutaga mayai mengi, kuwa na uzito mkubwa na nyama nyingi kwa umri mdogo.

Ufugaji bora utazingatia kuchagua kuku wenye sifa nzuri na kuwaacha waendelee na uzalishaji na wanaosalia wauzwe au wachinjwe waliwe.

Jumapili, 25 Julai 2021

Mashine ya kisasa ya kilimo ya kuzolea mbolea - Case IH Magnum 340 Hawe...




Jumamosi, 24 Julai 2021

Jinsi teknolojia ilivyobadili kilimo na ufugaji-New Technology Farming Machine, Amazing Farming Machine, Smart Farming t...



Teknolojia ya kilimo imekuwa kwa kiasi kikubwa. Kilimo kimekuwa cha kisasa sana siku hizi,haswa katika nchi zilizoendelea. 

Jumamosi, 17 Julai 2021

Jinsi ya kuvuna mahindi kwa njia ya jadi

Ujasiriamali huja na ubunifu,kitu ambacho kinaweza kuongeza tija kwenye kile unachofanya. Tazama ubunifu huu katika uvunaji wa mahindi.


Jumatano, 26 Desemba 2018

KUWA MILIONEA KWA KULIMA TANGAWIZI


Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China.


Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama chai, soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).


AINA ZA
TANGAWIZI 

Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo
hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica)
na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.

TABIA YA MMEA 
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi,
wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia
na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo
kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni
membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua
ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

HALI YA HEWA NA
UDONGO 
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya
kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji
mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25.
Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.

MMEA WA TANGAWIZI

UPANDAJI 
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande
vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika
urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya
tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700
cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi
inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha
sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza
kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima
kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi
au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa
uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale
kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua
magugu, kama simazine au round up hutumika.

Magonjwa na
wadudu: 
• Madoa ya majani yanayosababishwa na
viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta
zingiberi.
• Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na
viini viitwavyo Pithium spp
• Mizizi fundo; inasababishwa na
Meloidegyne spp.

UVUNAJI 

Tangawizi huweza
kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 6-10 baada ya kupanda, wakati majani yake
yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa
kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa
kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo
hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao,
mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza
kupatikana.

USINDIKAJI 

Tangawizi
ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi
iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine
huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa
mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa
zimechanganywa na sukari na/au chumvi au bila kuweka kitu chochote. Hata hivyo
tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.

GHARAMA ZA
UZALISHAJI NA MAPATO


Gharama ya hekari moja

Kukodi shamba Tshs.=100,000/=

Mbegu 200, 000/=


Kulima 100,000/=

Kupanda 100,000/=

Kupalilia x 4 @ 90,000/= jumla = 360,000/=

Mbolea / samadi 150,000/=

Jumla 1,010,000/=

Mapato kwa hekari.

Ekari moja ya maandishi inatajwa kutoa kilo 8,000 hadi 10,000. Katika hali halisi, kwa uzoefu wangu, ekari moja hutoa kati ya kilo 4000 hadi 6,000. Kutegemeana na kama umeandaa shamba kwa wakati, umefanya palizi kwa wakati, uwepo wa mvua za kutosha na hali ya rutuba ya shamba lako.

Ghalama hizi hutegemea sana na msimu zinaweza shuka au kupanda zaidi.





MASOKO





Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg.





Kwa masoko ya Tangawizi wasiliana nasi kwa simu namba 0675 117 151, nasi tutakutafutia msoko ya uhakika.



Alhamisi, 6 Desemba 2018

viatamishi (incubators)




Wafugaji wengi wanaonesha kuvutiwa na njia ya utotoleshaji wa mayai unaofanywa na mashine maalumu za kutotolesha mayai maarufu kwa jina la viatamishi (incubators) .Wengi wana kiu ya kutaka kujua gharama, faida, hasara na upatikanaji wa mashine hizi.Kwa kuthamini mchango wa wafuatiliaji wa website hii, nimelazimika kuitumia wiki hii kulielezea hili swala kwa upana wake.

.Viatamishi ni nini?   Hizi ni mashine maalumu zinazotumika kurahisisha utotoleshaji wa mayai ya aina zote  ya kuku wa asili na wale wa kisasa. Pia, inaweza kutumika kwa mayai ya kwale, bata na kanga.Mashine hizi hutofautiana ukubwa, lakini pamoja na tofauti hiyo, bado kila moja ina uwezo wa kutumia muda mfupi kutotolesha mayai, tofauti na muda anaoutumia kuku kuatamia hadi kupata vifaranga.Aina za viatamishiKwa jumla, mashine hizi zote zina kazi moja tu ambayo ni utotoleshaji, japo zimetofautishwa kwa mifumo yake ya kiuendeshaji.Mfumo wa kwanza unazijumuisha mashine zote zinazototolesha mayai kwa kujiendesha zenyewe(automatic).Mfumo wa pili unaziunganisha mashine zote zinazofanya kazi kwa kuendeshwa kwa msaada wa kibinadamu.

Mashine zinazojiendesha zenyewe zinatumika sana kibiashara kwa sababu zinarahisisha kazi tofauti na ilivyo kwa zile zinazoendeshwa na binadamu.Mashine hizi zina faida kubwa kwani si rahisi kuharibu mayai kutokana na kuwa na mashine ndani ambayo kazi yake ni kusaidia kutawanya joto kwenye mayai.Uzuri wake ni kwamba hata joto likizidi uwezekano wa kuharibu mayai haupo kwa sababu feni inasaidia kupunguza joto ndani ya mashine.Kundi la pili linajumuisha mashine zinazofanya kazi zake kwa kutumia uwapo wa mtu muda wote.Aina hii ya mashine hutumia upepo wa kawaida kuendesha zoezi la utotoleshaji, haina feni maalum lakupoza joto.Hii ina maana lazima mtu awe karibu na mashine wakati wote wa utotoleshaji ili aweze kufanikisha mchakato wote.Sifa za viatamishi Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa mashine hizi hazitofautiani sana, ukiachilia mbali ukubwa na mfumo wa uendeshaji. Zipo mashine zenye uwezo wa kutotolesha mayai mengi zaidi kwa pamoja, na nyingine kulingana naudogo wake zinalazimika kutotolesha mayai machache kwa muda mfupi pia.Kwa kawaida mashine nyingi za utotoleshaji hutumia umeme kidogo wa unaokadiriwa kuwa waVoltage:110V- 220V.Ukifanikiwa kupata mashine bora, unajijengea uhakika wa kutotolesha asilimia 95 ya mayai yote.

Unazijuaje mashine bora? Si jambo rahisi kuzijua mashine bora, lakini unaweza kutazama baadhi ya vitu muhimu kama vile tochi maalumu yenye uwezo wa kukagua uhai wa mayai yaliyomo ndani ya mashine.Zipo mashine zenye uwezo wa kila trei ya mayai kuwa na sehemu ya kuangulia vifaranga, kuangalia mfumo maalumu ‘full Automatic’ unaoweza kugeuza mayai, kudhibiti joto na unyevu ndani ya mashine.Jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha unatumia mashine yenye uwezo wa kutunza joto kwa muda wasaa sita mara baada ya umeme kukatika.

Viatamishi vya mafuta :Ni muhimu pia kueleza kuwa mbali ya nishati ya umeme, viko vitamishi vinavyoweza kujiendeshakwa kutumia nishati ya mafuta kama ya taa au petrol. Kwa kawaida aina hizi za viatamishi huwa na gharama ndogo.Kwa Watanzania na hata viwanda vidogo vimekuwa vikitengeneza aina hizi za viatamishi. Ni muhimu kutafuta taarifa za viatamishi hivi kutoka kwa wataalamu wa ufugaji au wafugaji wakubwa.