Jumamosi, 27 Mei 2017

Black Australorp ( Kuku Weusi wa Malawi)


Australorp wanastahimili mazingira tofauti, kama kuku wa kienyeji aliye zoeleka nchini Tanzania. Na ni wazuri kwa ufugaji huria, kwa kuwaachia nje wajitafutie chakula wenyewe. Ingawa wanajulikana kwa sifa yao ya utagaji mayai mengi, lakini kuku hawa wanafaa kwa nyama pia, kwani huwa na nyama nyingi sana (dual purpose chickens)

Kuku hawa huweza kumpatia mfugaji faida kubwa, kwani ni wazuri kwa biashara ya mayai na nyama pia. Hawana sifa nzuri ya kulalia mayai, lakini akilalia hutotoa vifaranga vingi, na ni wazuri kwa uleaji wa vifaranga hivyo.

Utagaji wao wa mayai unakaribia ule wa kuku wa kizungu. Kuku hawa ni wakubwa, wazito, na wanamvuto sana kuwaangalia. Wanapendeza pia kwa ufugaji mdogo, katika mazingira ya nyumbani. Wana michirizi ya kijani pale wanapomulikwa kwenye mwanga mkali wa jua.

Kwa wastani Black Australorp, hufikisha mayai 250 kwa mwaka, wakiwa katika mazimgira mazuri. Kuku hawa ni wapole na rafiki kwa binadamu. Black Australorp ni wagumu, hawapati magonjwa mara kwa mara, hivyo basi huvumilia magonjwa ya aina nyingi, na hawachagui chakula. Wanakula vyakula wanavyo kula kuku wengine wa kienyeji. Huanza kutaga wakiwa na umri wa miezi mitano na nusu hadi sita.

Jogoo hufikisha kilo 3.5 – 5.0 na
Temba/hen hufikisha kilo 3.0 – 3.7

kwa mahitaji ya aina hii ya kuku,wasiliana nami kwa simu namba o716 71729o,tuko kigamboni,dar es salaam

Related Posts:

  • HIZI NDIZO SABABU ZA KUKU WAKO KUDONOA MAYAI NA KUDONOANAKati ya mambo ambayo mfugaji anatakiwa kuwa nayo makini ni pamoja na tabia za kila siku za mifugo yake. Kuna wakati kuku wanakuwa na tabia za kudonoa na kula mayai,pia kudonoana wenyewe kwa wenyewe. Tabia hii si nzuri na si y… Read More
  • Black Australorp ( Kuku Weusi wa Malawi)Australorp wanastahimili mazingira tofauti, kama kuku wa kienyeji aliye zoeleka nchini Tanzania. Na ni wazuri kwa ufugaji huria, kwa kuwaachia nje wajitafutie chakula wenyewe. Ingawa wanajulikana kwa sifa yao ya utagaji mayai… Read More
  • viatamishi (incubators)Wafugaji wengi wanaonesha kuvutiwa na njia ya utotoleshaji wa mayai unaofanywa na mashine maalumu za kutotolesha mayai maarufu kwa jina la viatamishi (incubators) .Wengi wana kiu ya kutaka kujua gharama, faida, hasara na upat… Read More
  • Fahamu sifa, faida na changamoto za ufugaji kuku wa asiliKuku wa asili ni aina ya kuku ambao wamekuwepo nchini kwa muda wa miaka mingi na damu au koo zao hazikuchanganywa na aina yeyote ya kuku wa kienyeji. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbalimbali.Kwa kawaida ufugaji wa kuku wa as… Read More
  • Je, unafahamu sababu za kuku wako kutaga mayai madogo!Je, unafahamu sababu za kuku wako kutaga mayai madogo!Mara nyingi wakati tupofuga mifugo yetu, huwa tunategemea matokeo chanya. Kinyume na hapo basi kuna sababu inayozuia kufikia malengo yetu. Kuna wakati kuku wetu wa mayai h… Read More

3 comments:

  1. Nahitaji mbegu ya hawa kuku weusi je mnauza bei gani ?

    JibuFuta
  2. 1800 kwa kifaranga cha wiki mbili. Karibu kamembakilimo kwa maendeleo yako

    JibuFuta
  3. npo mbeya je nawezaje kupata hivyo vifalanga?

    JibuFuta