Jumatatu, 13 Agosti 2018

HIZI NDIZO SABABU ZA KUKU WAKO KUDONOA MAYAI NA KUDONOANA


Kati ya mambo ambayo mfugaji anatakiwa kuwa nayo makini ni pamoja na tabia za kila siku za mifugo yake. Kuna wakati kuku wanakuwa na tabia za kudonoa na kula mayai,pia kudonoana wenyewe kwa wenyewe. Tabia hii si nzuri na si ya kawaida. Hizi hapa chini ni sababu zinazopelekea kuku kuwa na tabia hizi:

SABABU ZA KUKU KULA MAYAI.

1. Ukoo- Hapa utakuta ndo ukoo/uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai,

2. Kuto kupata chakula cha kutosha- Hii ni moja ya sababu kubwa kabisa inayo pelekea kuku kula mayai,chakula kikiiwa kichache hawashibi hupeleka kutafuta njia mbadala ya kushiba. 

3. Kukosa madini joto- Hii inaweza kuwa ndo sababu kuu ya kwa nini kuku wanakula mayai, kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe, na jua kwamba kwenye yai kuku huwa anatafuta lile ganda la juu pekee sema anapo donoa na kulipasua yai hujikuta anakula na ute na kiini ila yeye lengo lake hasa ni ganda la juu.

 4. Kuku kutagia sehemu nyeupe sana yenye mwanga mkali upelekea kuku kula mayai,kuku anapenda kutagia sehemu fichifichi yenye mwanga hafifu kidogo ndo anakua huru zaidi kutaga.

5. Mayai kukaa muda mrefu bila kukusanywa baada ya kutaga- Hapa ni kwamba mayai yanapo kaa muda bila kukusanywa na kama yapo sehemu ya wazi ni rahisi wao kudonoa.

6. Lishe mbaya-kuku akipata lishe mbaya ya chakula humpelekea kudonoa chakula,kuku anapaswa kupata chakula chenye virutubisho vyote.

7. Nafasi ndogo-kuku wanapaswa kupata nafasi kubwa yakupumzika na kulia chakula.

8. Vyombo vichache-bandani unapaswa kuwa na vyombo vya chakula na maji vya vyakutosha kuondoa kusukumana na kutokula kwa raha.

9. Kukosa shughuli yakufanya-kuku wakila wakishiba unapaswa kuwafungia majani km kabeji ili wawe bize mda wote.

NAMNA YA KUZUIA KUKU KUDONOANA AU KULA MAYAI 

1. Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba.

 2. Mayai yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani. 

3. Sehemu ya kutagia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai alilo taga.

4. Madini joto ni muhimu sana. 

5. Kuku wenye tabia za kula mayai unaweza chinja au kuuza. 

6. Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehem ulionayo.

 7. Usizidishe mwanga. 

8. Banda liwe safi.

9. Weka vyombo vya kutosha. 

10. Wape lishe bora

11. Wape kuku shughuli kwa kuwawekea bembea na sehemu ya uwazi kwa ajili ya mazoezi. 

12. Kata midomo ya juu.

13.Epuka ukoo wenye tabia hizo.

Kwa leo naishia hapa,nakutakia mafanikio mema kwenye ujasiriamali wako, Mungu awabariki sana.
⁠⁠⁠

Related Posts:

  • Magonjwa ya kuku, Dalili, kinga na tiba zakeMagonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa … Read More
  • Mtaji wa kufuga kuku wa kienyeji, mchanganuo wake na namna ya kupata sokoPengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye… Read More
  • NJIA BORA ZA UTUNZAJI WA MAYAI YA KUKUKwa kawaida kuku huanza kutetea(Kutoa mlio wa ishara ya kutaga) anapofikisha miezi sita hadi minane. Hivyo ni vyema viota viandaliwe mapema wakiwa na umri wa miezi mitano. Kuku anapoanza kutaga akifikisha mayai matatu mfugaji… Read More
  • ULISHAJI WA KUKU WA MAYAIULISHAJI WA KUKU WA MAYAI (LAYERS)Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri. Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri k… Read More
  • UTUNZAJI WA VIFARANGA(KUKU WA KIENYEJI NA WA MAYAI)Utunzaji wa vifaranga:- siku ya kwanza waweke katika brooder(banda la kuku)wape glucose kwa masaa sita hadi nane ya kwanza kurudisha nguvu iliyo poteabaada ya kuwapa glucose wape Esb3 au S-dime au amprolium kwa siku 1-3Siku y… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni