Alhamisi, 16 Machi 2017

MAAJABU YA MAFENESI ( ARTOCARPUS HETEROPHYLLUS LAM)


MAFENESI au Jackfruits kwa lugha ya kiingereza na majina mengine Langka na Nangka ni matamu kwa ladha yake. Lakini pia yana umuhimu katika mwili wa binadamu.

Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats).

Lakini kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na Tanzania,

Na nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Mbeya(Kyela) nk.

Na sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.

Mafenesi yana vitamin B1 na B2, vitamin C, flavonoids na ni chanzo kizuri cha carotenoids na Potassium nk. Katika nchi kama Thailand majani machanga na maua machanga ya kiume hupikwa kama mboga. Matunda yaliyoiva hulimwa yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa na nazi au hutengeneza ice cream, chatine(chutney), jam, jeli, (jelly) na pesti.

Mfenesi una faida nyingi tukianzia na majani hutibu homa  magonjwa ya ngozi majipu, vidonda na kisukari. Tunda lina wingi wa vitamin C ambayo kiafya inasaidia kuongeza kinga ya mwili, tunda hili linasaidia kupunguza mafua, kifua na homa. Vitamin C hiyo husaidia kuondoa sumu mwilini na kuukinga mwili na maradhi pale linapotumiwa ipasavyo.

Fenesi pia linasaidia kuupa mwili nguvu kwani lina madini ya wanga na sukari ambayo husaidia kuupa mwili nguvu kwa haraka. Fenesi linaweza kuondoa sumu mwilini hivyo linakinga na saratani za aina mbalimbali kama ile ya mapafu. Mdomo na kinywa  na tumbo. Fenesi hutia nguvu mwili na kwenda haja vizuri. Kwa wale wenye matatizo ya shinikizo la damu, Fenesi ni tiba nzuri kwani ina madini ya potassium ambayo husaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza uwezekano wa kupata  shinikizo la damu na kukuondoa katika hatari ya kupata kiharusi. Mizizi yake hutibu homa, kuharisha, magonjwa ya ngozi  na asthma. Utomvu wake ukichanganywa na siki hutibu tambazi (abscesses), kuumwa na nyoka na uvimbe wa tezi (glandular) nk. Magamba yake hutibu vidonda kwa kuweka kibandiko (poultices)

Mbegu zake zikikaangwa huongeza tendo la kujamiiana.

Watanzania tuanze kula fenesi baada ya kula husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula kwa sababu ni tunda muhimu na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa. Pia kwa wenye matatizo ya macho na kutokuona vyema, tunda hili ni mkombozi mkubwa  kwani lina wingi wa vitamin C ambayo huongeza kiwango cha kuona (uoni), pia lina uwezo wa kuondoa sumu, hufanya kazi katika retina na kuifanya iwe imara.

 

Related Posts:

  • KILIMO CHA BAMIA BAMIAAsili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.Urefu wa mmea huwa kati ya meta mo… Read More
  • KILIMO BORA CHA VITUNGUUKITUNGUU-ONION (Allium cepa)Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlowa familia za kitanzania. Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katikamatumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumikaka… Read More
  • KUWA MILIONEA KWA KULIMA TANGAWIZITangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili … Read More
  • KILIMO CHA MATANGOni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°CUdongo Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha majiMaandalizi ya shamba Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe … Read More
  • Kilimo Bora Cha Pilipili HohoJina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha.Kilimo hiki kinaende… Read More

0 comments:

Chapisha Maoni