• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Jumatano, 29 Machi 2017

UFUGAJI WA SAMAKI


Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).


Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

Jumatatu, 27 Machi 2017

ULISHAJI WA KUKU WA MAYAI

ULISHAJI WA KUKU WA MAYAI (LAYERS)


Kuku wa mayai ili watage vizuri wanatakiwa walishwe chakula bora kwa utaratibu unaotakiwa, ukiwazidishia au kuwaongezea hawatotaga vizuri. Wanatakiwa walishwe kati na kati kulingana na umri kama ifuatavyo:-

UMRI WA WIKI 1 -2
Katika umri huu wanapewa chakula aina ya "Super Starter" kwa ajili ya kuwatengenezea kinga mbadala ili waweze kuhimili mikiki mikiki ya vijidudu vya magonjwa kadri wanavyoendelea kukua, wanapewa chakula hicho kwa kiwango maalum kama ifuatavyo:-
Wiki ya 1: Gramu 12 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 2: Gramu 22 kwa kuku mmoja kwa siku moja


UMRI WA WIKI 3 - 8
Hapa wanakuwa bado ni vifaranga na wanapewa chakula aina ya "Chick Starter" kwa ajili ya kuendelea kuwajenga miili yao waweze kupoekea virutubisho vizuri, hii inatokana na kwamba kuna baadhi ya viinilishe vinafanya kazi ya kumeng'enya chakula na kupatikana viinilishe vingine, kwahiyo vikikosekana katika mwili wa kuku basi hata wale chakula gani bora, hawawezi kutoa mazao bora, lakini kwa kuwapa "Chick Starter" itawapelekea kuwa na virutubisho hivyo muhimu. Kiwango na ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 3: Gram 27 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 4: Gram 32 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 5: Gram 38 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 6: Gram 42 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 7: Gram 46 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 8: Gram 50 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 9 - 18
Katika umri huu kuku wanapewa chakula aina ya "Grower Mash" kwa ajili ya kuwakuza na kuwajenga mfumo wa uzazi kwa maandalizi ya utagaji. Kiwango cha chakula kinategemea na wiki kama ifuatavyo:-
Wiki ya   9: Gram 56 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 10: Gram 62 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 11: Gram 64 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 12: Gram 66 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 13: Gram 68 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 14: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 15: Gram 74 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 16: Gram 80 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 17: Gram 82 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 18: Gram 88 kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 19 - 40
Huu ni umri ambao kuku wanataga kwa kiwango kikubwa sana (85% hadi 100%) hali ambayo inawafanya kutumia nguvu nyingi mno, hivyo hupewa chakula aina ya "Layers Phase 1" kwa ajili ya kufidia nguvu ya ziada wanayotumia ili waendelee kutaga kwa kiwango hichohicho. Ulishaji wake ni kama ifuatavyo:-
Wiki ya 19: Gram 92 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 20: Gram 102 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 21: Gram 108 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 22: Gram 114 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 23: Gram 116 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 24: Gram 120 kwa kuku mmoja kwa siku moja
Wiki ya 25 - 40: Gram 130  kwa kuku mmoja kwa siku moja

UMRI WA WIKI 41 - 80
Katika umri huu kuku wanakuwa wameanza kuchoka na huanza kutaga kwa kiwango cha kawaida (65% hadi 75%) hivyo hupewa chakula aina ya "Layers Phase 2" kwa ajili kuendeleza (maintain) kiwango chao hicho kwa muda mrefu. Kiwango chao ni "Gram 130 kwa kuku mmoja kwa siku moja".


NB: Kuanzia wiki 81 na kuendelea unaweza kuwauza na kuweka kuku wengine.

Jumatano, 22 Machi 2017

JINSI YA KUONGEZA RUTUBA KWENYE SHAMBA LAKO

Ili kuvuna mazao mengi lazma udingo unao lima uwe na rutuba ya kutosha ili kusababisha mazao yako kupata virutubisho muhimu kwa ukuaji
zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia mkulima kuongeza rutuba kwenye shamba lako

  usipande mazao ya aina moja kwa mfululizo, hautakiwi kupanda mazao ya aina moja mfano mahindi na mtama kwa kufuliuliza ili kuepusha virutibisho kupotea vyote  na itasababisha magonjwa na wadudu kuwa wengi shambani

usitumie mbolea za kemikali mara kwa mara,hii pia haitakiwi, mbolea za kemikali mfano UREA hua hazitajkiwi kutumika mara kwa mara husababisha alzi kupunguza rutuba mbolea hizi utumika mara moja moja zinapo itajika.

usipende sana kuchoma shamba, unapo choma shamba unasababisha kuuwa wadudud wanao sababisha kuongeza rutuba kwenye udongo na pia huua uoto asiri.

zika mabaki ya mazao baada ya kuvuna, unapo vuna mabaki ya mazao mfano mabua yanapo zikwa na kuoza husababisha kuongeza rutuba kwenye udongo husika.

panda mazao ya jamii ya mikunde, pia mazao ya mikunde mfano kunde na maharage husaidia kuongeza naitrogen ambayo inatakiwa sana na mimea hivo rutuba huongezeka

weka mbolea ya samadi ,hii ni mbolea hasiri inayo yani ni kinyesi cha ng'ombe hivo ili kuongeza rutuba inabidi uweke sana samadi kwenye shamba lako hii itasaidia sana kurudisha rutuba kwenye shamba lako.

pumzisha shamba, Wakulima wengi hua hawapendi kupumzisha shamba hivo wanashauliuwa kupumzisha shamba kwa mda hii usaidia shamba kuongeza rutuba iliyo kua imepotea.

usitumie sana viuagugu,hii pia ni mbaya kutumia ke mikali za viuagugu badala yake palilia kwa jembe na badae yazike magugu ili rutuba iendelee kubaki kwenye shamba lako.

usitifue kupita kipimo, hii husababisha mmomonyoko wa udongo na pia rututba nyingi hupote kwa huo mmomonyoko

KILIMO BORA CHA VITUNGUU


KITUNGUU-ONION (Allium cepa)

Vitunguu ni zao la pili ambalo hutumika karibu kila siku katika mlo
wa familia za kitanzania. Vitunguu vina chukua nafasi kubwa katika
matumizi ya mboga hasa kwa wakazi wa mijini. Vitunguu hutumika
katika kutengeneza kachumbari, kiungo cha mboga, nyama na
samaki. Majani ya kitunguu hutumika kama mboga. Vitunguu pia
hutumika kutengeneza supu. Vitunguu huweza kutoa Tani 10 hadi 16 Kwa ekari (magunia 80 hadi 160).

HALI YA HEWA NA UDONGO UFAAO KWA KILIMO CHA VITUNGUU
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye maeneo yasiyo na mvua
nyingi sana, yenye baridi kiasi wakati wa kiangazi na yasiyo na joto
kali pamoja na ufukuto wa ukungu wakati wa kukomaa vitunguu.
Zao la vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya
kutosha. Udongo unao ruhusu mizizi kupenya kirahisi, unao hifadhi
unyevu kama vile udongo wa mfinyanzi tifutifu.
Upandaji wa mbegu za vitunguu
Hapa Tanzania upandaji wa mbegu za vitunguu katika kitalu kwa
ujumla huanza mwezi machi hadi mei kutegemea na msimu wa
kilimo. Hivyo kilimo hiki hufanyika  mara baada ya mvua za masika
kubwa kuisha. Kipindi cha kiangazi na baridi huruhusu ukuaji mzuri
wa vitunguu. Kiasi cha Kilogram 1.5 hadi 2 za Mbegu Hutosha kwa ekari moja.
Mbegu za vitunguu huoteshwa mapema katika kitalu. Mbegu
zinaweza kupandwa kwa mstari au kwa kutawanya katika tuta la
kitalu. Katika upandaji wa mstari, mbegu hupandwa katika nafasi
ya sm 10 hadi 15 kati ya mstari na mstari.
Baada ya kupanda, mbegu hufunikwa kwa udongo na baadaye
kwa kuweka matandazo juu ya tuta. Mara baada ya mbegu kuota,
matandazo yaondolewe na badala yake kichanja cha nyasi
kijengwe ili kuiwekea kivuli mimea michanga. Mbegu huota baada
ya siku 7 hadi 10.www.kilimofaida.blogspot.com

KUPANDIKIZA MICHE YA VITUNGUU BUSTANINI
Upandikizaji wa miche ya vitunguu bustanini hufanyika baada ya
miche kukua na kufikia ukubwa wa unene wa penseli. Mara nyingi
miche hii itakuwa imesha kaa kitaluni kwa siku 40 baada ya mbegu
kupandwa.
Usichelewe kuhamisha na kupandikiza miche hii bustanini. Kwa
sababu miche mikubwa sana itaweza kutoa maua badala ya kutoa
tunguu. Na hivyo mara nyingi vitunguu namna hii hubaki na suke la
maua.
Wakati wa kupandikiza miche haishauriwi kukata wala kupunguza
majani. Miche ipandikizwe katika nafasi ya sm 30 kati ya mstari na
mstari na sm 10 kati ya mche na mche.


Upandaji wa miche bustanini unaweza kufanyika kwenye  mistari
katika matuta au kwenye vijaruba. Vijaruba vya mraba hutumika
kwenye maeneo yenye ardhi tambarare na iliyo kame ili kuhifadhi
maji baada ya kumwagilia. Kwa sehemu zenye udongo mzito na
zenye maji mengi tumia matuta yenye mwinuko wa sm 10 hadi sm
15 kutoka usawa wa ardhi.
Matunzo ya bustani ya vitungu.

UMWAGILIAJI
www.kilimofaida.blogspot.com
Zao la vitunguu linahitaji maji ya kutosha katika kipindi chote cha
ukuaji wa mmea na hasa wakati wa kutunga tunguu.
Katika kipindi kisicho na mvua (mwezi mei hadi Agosti) umwagiliaji
ufanyike mara moja kwa wiki kwa udongo wa mfinyanzi tifutifu na
vitunguu vilivyopandwa katika vijaruba.
Ili kuharakisha kukomaa kwa vitunguu unashauriwa kupunguza
kiasi cha maji ya kumwagilia taratibu kadri zao linavyo kua. Pia ni
vizuri uache kumwagilia maji mapema wiki nne hadi sita kabla ya
kuvuna. Kwani muda kamili wa kukomaa na kuvuna kwa vitunguu
ni siku 90 hadi 150 kutegemea na aina ya mbegu.
Kuthibiti magugu na kupandishia udongo
Kitunguu ni zao lisilo weza kushindana na magugu. Magugu
husababisha kupungua kwa ukubwa wa kitunguu, hueneza
magonjwa na husababisha kudumaa kwa vitunguu.
Katika bustani ya vitunguu, magugu yanaweza kutolewa kwa njia
ya kutifulia kwa jembe dogo, kung'olea kwa mkono na pia kwa
kutumia madawa ya kuua magugu.
Kama unaondoa magugu kwa kutifulia, epuka kutifua kwa kina
kirefu ili kutoharibu mizizi na vitunguu vyenyewe, kwani mizizi ya
vitunguu ipo juu juu sana.
Kupandishia udongo kwenye mashina ya vitunguu ni hatua
muhimu ili vitunguu visiunguzwe na jua. Hakikisha kuwa
mashina ya vitunguu vyako ndani ya udongo kama
sentimita 5. Pia kuna aina ya vitunguu ambavyo hutoa au
hupandisha tunguu lake juu ya udongo wakati vinapokua.
Hivyo kupandishia udongo ili kufunika tunguu ni muhimu
sana.


MAGONJWA YA VITUNGUU NA WADUDU WAHARIBIFU

WADUDU WAHARIBIFU

Kuna aina tatu za wadudu wanao haribu zao hili:

1>Viroboto wa vitunguu
Hawa ni wadudu waharibifu namba moja wa zao la vitunguu hapa
nchini Tanzania. Husababisha upotevu mkubwa wa mavuno.
Wadudu hawa huonekana hasa wakati wa kipindi cha joto.
Dalili za kugundua
Majani yaliyo shambuliwa na wadudu hawa huwa na mabaka
meupe yenye kung'aa. Katika hali iliyo kithiri majani yote hugeuka
kuwa na tabaka nyeupe au kijivu cheupe na baadaye majani
hunyauka kabisa.
Kuzuia

Mdudu huyu huzuiwa kwa kupiga dawa kama vile thiodan-35,
Parathion nk.

Ili kupunguza uvamizi mkubwa, panga upandaji wa vitunguu
mapema ili kipindi cha joto kiingiapo zao lako liwe limekomaa.

Epuka kupanda zao la vitunguu sehemu iliyo kuwa na mazao
aina ya vitunguu kama vile liksi, vitunguu swaumu, n.k.

2> funza na minyoo ya mizizi
wanakata miche .

Hawa hupigwa vita kwa kuzingatia mzunguko wa mazao
bustanini.

MAGONJWA YA VITUNGUU

a) Ukungu mweupe
Ugonjwa huu hujionyesha kipindi cha baridi iliyo ambatana na
unyevunyevu mwingi hewani.
Dalili za kugundua Ugonjwa huu

Utaona unga unga wa rangi ya zambarau katika majani.

Majani hugeuka rangi na kuwa njano na baadaye
kunyauka.

Ugonjwa huu hupenya hadi chini kwenye tunguu na
kusababisha kuoza kwake.
Kuzuia

Unashauriwa kubadili aina ya zao katika shamba lako
kwa kupanda mazao mengine yasiyo jamii ya vitunguu.
Kilimo cha mzunguko wa aina mbalimbali za mazao
upangwe kiasi kwamba vitunguu visipandwe eneo moja
mpaka baada ya miaka 3 kama ugonjwa ulikuwa
mwingi.

Tumia dawa za kuzuia ukungu. Hii ifanyike kabla ya
kuona dalili za ugonjwa kwenye vitunguu. Piga dawa
kama vile maneb, dithane M45, zineb ya unga, n.k.
Wakati unapoona hali ya hewa inayo wezesha kuenea
kwa ugonjwa huu (yaani baridi iliyo ambatana na
unyevunyevu mara kwa mara). Katika kipindi hiki piga
dawa kila baada ya siku sita ili kuzuia kuingia kwa
ugonjwa. Ugonjwa ukisha ingia kwenye mimea
hauzuiliki kwani hakuna dawa ya kuponyesha.

b) Ukungu wa kahawia
Ugonjwa huu unaweza kuleta madhara makubwa wakati
vitunguu vikiwa bustanini na hata wakati vikiwa katika ghala.


Dalili zake
Vikovu vya mbonyeo hujitokeza kwenye majani na baadaye
hutoa doa la rangi ya zambarau. Vikovu hivi hukua na
kutengeneza vidonda ambavyo hukua na kufanya mzunguko
katika jani zima au shina la kitunguu. Baada ya wiki kama tatu
hivi tangu kuingia kwa ugonjwa huu, majani yote huanguka na
kukauka.
Ugonjwa huu hushambulia vitunguu hata baada ya kuvuna kwa
kupitia shingo ya kitunguu au sehemu yoyote yenye kovu,
kidonda au mkwaruzo.
Namna ya kuzuia

Katika bustani, mara uonapo kitunguu chenye dalili za
ugonjwa huu, ondoa mimea na kuiteketeza kwa moto ili
kuzuia au kupunguza kuenea kwa ugonjwa.

Kwa kinga ya bustani, piga dawa za Dithane M 45 na dawa
zingine za kuzuia magonjwa ya ukungu. Dawa hizi zitasaidia
kupunguza kutawanyika  kwa ugonjwa.

Tumia kilimo cha kuzungusha au kubadilisha mazao katika
eneo la bustani yako. Usipande mfululizo jamii yoyote ya
vitunguu katika shamba ulilovuna vitunguu.

Wakati wa kuvuna, epuka kukata au kusababisha vidonda
katika vitunguu, yaani vuna kwa kung’olea na siyo kwa
kuchimba na jembe.

Baada ya kuvuna anika vitunguu juani kwa siku moja au mbili
kabla ya kuviweka katika magunia au ghala.

c) Ugonjwa wa kuoza mizizi
Huu ni ugonjwa unaotoka udongoni na unasababishwa na
vimelea vya jamii ya ukungu.
Dalili
Dalili za ugonjwa huu ni mizizi kugeuka rangi na kuwa njano na
baadaye kuwa zambarau. Baada ya muda ugonjwa huenea na
mizizi hufa kwa kunyauka. Majani nayo hugeuka kuwa na rangi
ya njano na kisha shina au mche mzima hunyauka.
Kuzuia

Tumia kilimo cha kuzungusha mazao badala ya kupanda
vitunguu katika eneo moja toka msimu moja hadi
mwingine.

Panda aina za vitunguu zinazo vumilia ugonjwa huu kwa
mfano: Excel, L 36, Granex, White Granex na red creole.
Uvunaji wa vitunguu
Kwa ujumla uvunaji vitunguu hufanyika baada ya siku 90 hadi
150 tangu kupanda kwa miche yaani miezi mitatu hadi mitano
tangu miche kupandikizwa bustanini.
Utagundua kuwa vitunguu viko tayari kuvunwa baada ya kuona
kuwa karibu asilimia 50 au nusu ya mimea shambani inaanza
kuanguka na majani kukauka.
Ili kurahisisha ukaushaji na hifadhi sahihi ya vitunguu, pangilia
vizuri msimu wa kupanda ili kwamba uvunaji ukutane na kipindi
cha joto na kiangazi.
Uvunaji ufanyike kwa kung'oa baada ya kumwagilia maji bustani
siku moja kabla ya kuvuna.
Baada ya kuvuna kata majani kama sentimeta 2 juu ya tunguu.
Pia kata mizizi mirefu kwa sm 2 (usikate chini sana ya shingo
wala kitako cha kitunguu kwani hii husababisha kuoza kwenye 26
ghala au gunia la kusafirishia na kuenea kwa magonjwa. Baada
ya hapo kitunguu kianikwe juani kwa siku 1 hadi 2.
Vitunguu vilivyo anikwa vizuri ni vigumu kwa kubonyeza kwa
kidole gumba pia shingo ya kitunguu huwa kavu.
Mavuno ya vitunguu vilivyo tunzwa vizuri yaweza kufikia tani 7
hadi 10 kwa hecta.
Baada ya kuvuna na kuanika:

Chagua vitunguu vizuri, tenga vibovu na vilivyo vidogo
sana

Ondoa vitunguu vilivyo na makovu pamoja na vile vyenye
shingo nene (shingo ya chupa).

Undoa maganda yanayo pepea ovyo.
Baada ya uchambuzi huu, hifadhi vitunguu kwenye ghala kama
husafirishi na kama unasafirisha pakia vitunguu katika magunia
yenye kupitisha hewa ya kutosha.
Katika ujazaji wa magunia usishindilie na wala usiweke
vitunguu vichache katika gunia. Kushindilia sana vitunguu
hubabisha mkandamizo mkubwa na hivyo kuoza kwa vitunguu,
na usipojaza vizuri vitunguu katika magunia hutokea msuguano
wakati wa kusafirisha na hivyo kusababisha vidonda vitakavyo
fanya vitunguu kuoza.
Kama vitunguu havisafirishwi kwa ajili ya soko, vinaweza kutunzwa
katika sehemu kavu
iliyo na mzunguko mzuri wa hewa ya kutosha.
Vitunguu kama vile aina ya Red Creole na Texas Grano
vinahifadhika vizuri. Kwa vitunguu vilivyo hifadhiwa vizuri, huweza
kudumu hadi miezi 6 bila kuharibika. Kwa sehemu zilizo na joto
kali, usihifadhi vitunguu zaidi ya miezi mitatu kwani vitunguu
huanza kuoza na au kuchipua.
Picha ya vitunguu vya Red Creole

Image result for picture of red creole onion

Picha ya vitunguu vya texas Grano

Image result for piCTURE OF TEXAS GRANO ONION

Jumatatu, 20 Machi 2017

KILIMO CHA MATANGO

ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C

Udongo Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji

Maandalizi ya shamba Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45


Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta

Upandaji Zipo aina mbili za upandaji,
1.ya kwanza ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja na

2. ya pili ni ile ya kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.

Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi

Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda

Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda



Palizi Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu.



Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani ‘plastic mulch’

Mbolea Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda na kisha tumia NPK yenye uwiano mmoja kama, 18:18:18, 17:17:17 ama 16:16:16 baada ya wiki tatu toka Usegekaji
Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza

Uchavushaji
Hii ni muhimu sana kuzingatiwa kwani tango huchavushwa kwa wadudu na si upepo
.Bila wadudu kama nyuki uzalishaji huathrika sana.

Ni muhimu kupanda mazao kama alizeti na maua mbali mbali yanayopendwa na wadudu wachavushaji ili kuhakikisha uwepo wa wadudu hao shambani.

Aidha inapo-lazimu ni vema kuweka mizinga kadhaa ya nyuki katika shamba la tango

Mavuno  huanza baada ya siku 40 hadi 45 kutegemea na aina pamoja na hali ya hewa

Jumamosi, 18 Machi 2017

Magonjwa ya kuku, Dalili, kinga na tiba zake


Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle(kideli)
Ugonjwa huu ndio huathiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%.

Dalili za kwanza
ni shida ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate.

Dalili
• Kuhalisha choo cha kijani na njano
• Kukohoa na kupumua kwa shida
• Kuficha kichwa katikati ya miguu
• Kukosa hamu ya kula na kunywa
• Kutoa kamasi na machozi
• Kupooza na kuzungusha kichwa na kutembea kinyumenyume
• Idadi kubwa ya vifo hadi 90%

Kinga
•Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
• Epuka kuingiza kuku wageni
• Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
• Zingatia usafi wa mazingira

Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia.

Tiba
Ni bora basi kutibu minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya nipiperazine, phenothiazine na butynorate.

Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur audawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu

Wadudu kama viroboto,Utitiri na chawa
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri husababisha harara ya ngozi, kuku walio athiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.

Tiba
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa matundu) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku150).

Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.

Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.

  •  Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia

  •  Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa

  •  Nyunyiza dawa kwenye viota

  •  Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku

  • Fuata kanuni za chanjo

  •  Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima


Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huathiri njia inayopitisha hewa na kuambatana mate na sauti kama ya kikohozi.

Dalili
Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji wake pia hutokea polepole na vifo sio kwa wingi. Hata hivyo, Tatizo hili laweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga walipoanguliwa hadi pale walipouzwa.

Tiba
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha milligram 35 ya tylosin hutosha kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii hukomesha madhara yanayotokanana magonjwa ya mapafu.

Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakatimmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya gramu 4.

Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.

Ndui ya kuku/ fowl pox
Ndui huathiri sana vifaranga wanaokua hasa wakati wa mvua, Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu. Ugonjwa huu husababishwa na virusi na hauna tiba

Dalili
• Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana kama kishungi,usoni na chini ya mdomo
• Kukosa hamu ya kula
• Vifo vingi

Kinga
• Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
• Epuka kuingiza kuku wageni
• Zingatia usafi wa mazingira

Ukosefu wa vitamin A
Huathiri zaidi kuku wadogo wanaokua,

Dalili
macho huvimba na kutoa uchafu mzito kama sabuni ya kipande iliyolowa maji,
kuku wenye ukosefu wa vitamin A hawaponi na hatimaye hufa.
Mara kwa mara ugonjwa hujitokeza wakati wa kiangazi,

kinga 
ni kuwapa kuku mchicha au majani mabichi mara kwa mara pia wape kuku wote dawa ya vitamin za kuku zinazouzwa maduka ya mifugo ili kuzuia kujitokeza kwa ugonjwa huu.

Mafua ya kuku/infectious coryza
Hutokana na bakteria na hushambulia hasa kuku wakubwa

Dalili
• Kuvimba uso
• Kamasi zilizochanganyikana na usaha unaonuka
• Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
• Hukosa hamu ya kula
• Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya

Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamin
Kuhalisha damu/coccidiosis
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa

Dalili
• Kuharisha damu
• Manyoya husimama
• Hulala na kukosa hamu ya kula
Homa ya matumbo/fowl typhoid
• Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
• Kuku hukosa hamu ya kula
• Kuku hukonda
• Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
• Kinyesi hushikamana na manyoya

Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini

Kinga
• Usafi
• Fukia mizoga
• Usiingize kuku wageni
• Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6

Kilimo Bora Cha Pilipili Hoho



Jina la kitalaamu la PILI PILI HOHO ni Capsicum annum. Asili ya zao hili ni bara la Amerika ya Kusini. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Iringa, Tanga (Lushoto), Mbeya, Ruvuma, Tabora na Arusha.

Kilimo hiki kinaendeshwa na wakulima wadogo katika maeneo yenye ukubwa wa kati ya hekta 0.2-0.4 pia kuna maeneo ya wakulima wakubwa wenye hekta kati ya 2-20. Wakulima hao hujishughulisha na kilimo cha zao hilo kwa njia ya mkataba na kampuni hiyo.

Hoho hutumika katika kutengeneza rangi za asili za vyakula ambazo kwa sasa hupendwa zaidi kuliko zile zinazotokana na kemikali na pia huongeza ladha na harufu katika vyakula.

Hivyo hutumika katika viwanda vya kusindika vyakula, kwa mapishi ya nyumbani na hata katika viwanda vya vipodozi kama rangi ya mdomo, uso n.k. Ina virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kama madini ya chuma, vitamin A na C.


2.0 TABIA YA MMEA 
Hoho ni zao la jamii ya pilipili isiyo kali, tunda lake ni nene kiasi la duara pia linaweza kuwa lililochongoka,.

3.0 ENEO NA HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO 
Hoho hustawi vema katika maeneo ya usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2,000 yenye mvua ya wastani wa mm.600-1,250 na wastani wa joto la nyuzi za sentigredi 21 hadi 24.

Udongo wa tifitifu wenye rutuba, usiotuamisha maji na wenye hali ya uchachu (pH) kati ya 5.0-6.5 hufaa zaidi. Umwagiliaji ni muhimu pale mvua inapokuwa chache.

4.0 UZALISHAJI 

4.1 UTAYARISHAJI WA KITALU 
Chagua eneo katika ardhi isiyo na mtelemko mkali na yenye rutuba ya kutosha. Ardhi iwe imepumzishwa bila kuoteshwa mazao ya jamii ya pilipili, biringanya, nyanya, n.k. ili kuepukana na mashambulizi ya wadudu na magonjwa.

Tayarisha kitalu kabla ya msimu wa mvua. Andaa vizuri matuta manne yenye urefu wa wastani wa mita 10 kila moja na upana wa mita moja (1) ili kustawisha miche inayotosha ekari moja.

Acha njia ya nusu mita kati ya tuta na tuta. Mwagilia maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu na endelea kunyweshea kulingana na hali ya hewa na hali ya udongo.

Sia mbegu kwenye, mstari, nafasi kati ya mstari na mstari ni sm 10 na kina cha sm1. Kiasi cha mbegu cha nusu kilo kinatosha eneo la hekta moja.

Weka matandazo kwenye kitalu au tumia nailoni nyeusi ili kuhifadhi unyevunyevu na kuzuia uotaji wa magugu.

4.2 UTAYARISHAJI WA SHAMBA 
Shamba lilimwe vizuri na kuweka matuta ili kuhifadhi unyevunyevu na kurahisisha umwagiliaji.

Matuta yanaweza kuwa makubwa au madogo kulingana na matakwa ya mkulima. Matuta makubwa hupandwa mistari miwili na matuta madogo hupandwa mstari mmoja.

4.3 UPATIKANAJI WA MBEGU
Mbegu ambazo hutumika ni chotara ambazo huuzwa kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchi nzima.

Haishauriwi kutumia mbegu kutoka zao la msimu uliopita kwani ubora wa paprika utaharibika na hivyo kuharibu soko unashauriwa kununua mbegu bora.

4.4 UPANDAJI 
Mbegu huoteshwa na kukuzwa kitaluni kwa muda wa wiki 6-8 na miche hupandikizwa shambani ikiwa na urefu wa sm.6-10. Mwagilia maji kitaluni kabla ya kuhamisha miche.

Panda shambani kwa nafasi ya sm.75-90 kati ya miche kwa sm.90-105 kati ya mistari, wastani wa miche 12,500 itapatikana kwa hekta.

Weka samadi shambani tani 25-37 kwa hekta wiki 1-2 kabla ya kupandikiza miche, au kilo 560-670 za NPK (mbolea ya viwandani) kwa hekta kwa uwiano wa 4:7:7 katika udongo usio na rutuba ya kutosha.

5.0 KUHUDUMIA SHAMBA 
Palizi ifanyike mara magugu yanapotokea shambani. Umwagiliaji maji ufanyike kama ilivyo kwa mazao mengine kama nyanya.

Tumia mbolea kiasi cha kilo 140 za SA au CAN kwa hekta hasa wakati mmea inapotoa matunda ili kupata matunda makubwa na kuvuna kwa muda mrefu (hadi miezi 10).

6.0 MAGONJWA NA WADUDU 
Wadudu
• Funza wa vitumba
• Vidukari
• Kidomozi (Leaf miner)
Kudhibiti: Tumia dawa aina ya permethrin Magonjwa 


• Kuoza mizizi
• Mnyauko wa majani
• Batobato
Kudhibiti: Choma nyasi kwenye kitalu kabla ya kusia mbegu. 
Badilisha mazao yasiyo ya jamii ya pilipili. 

7.0 UVUNAJI 
Matunda ya kwanza huwa tayari kuvunwa kuanzia miezi 2-3 baada ya kupandikizwa; matunda yaliyokomaa vizuri na kuwa na rangi nyekundu ndiyo huvunwa. Matunda 30-80 hupatikana kwa mmea mmoja.

Ubora wa hoho huongezeka kutegemeana na kiwango cha rangi yake ikiwa ni nyekundu njano au kijani. Mazao kiasi cha tani 3.5 kwa hekta hupatikana.

Baada ya kuvuna mwagilia maji, piga dawa (kama ni muhimu) na weka mbolea kuongeza uzalishaji unaofuata.

8.0 USINDIKAJI 
Hoho huuzwa ikiwa bado fresh tofauti na jamii nyingine za pilipili ambazo zinaweza kukaushwa na kusindikwa kasha kuuzwa baadae.


9.0 SOKO LA PAPRIKA 
Soko la hoho lipo nchi nzima kwenya masoko makubwa na hata magengeni, hoho hutumiwa zaidi kama kiungo cha kupikia mapishi mbali mbali au kutia kwenye kachumbari.

Tatizo kubwa wanalokabiliana nalo wakulima ni kutokuwa na soko la uhakika ndani na nje ya nchi, mazao huweza kuoza shambani au njiani kutokana na tabu ya usafiri hasa vijijini ambapo mvua zikinyesha barabara hazipitiki kwa urahisi

Kuna aina ya pilipili isiyo kali kama hoho lakini ni ndefu kama pilipili za kawaida ijulikanayo kama PAPRIKA ambayo ina soko kubwa nje ya nchi.

Zao hili kwa sasa huzalishwa kwa msukumo wa kampuni ya kigeni ya Hispania inayoitwa Tanzania Spices Ltd iliyopo mkoani Iringa


10.0 GHARAMA YA UZALISHAJI WA HEKTA MOJA: 
Mbegu Tshs. 24,000 /-
Vibarua 200,000/-
Mbolea(mboji/samadi) 300,000/-
Madawa 100,000/-
Jumla 624,000/-

MAPATO: 
Kilo 3,500/- X 800/- 2,800,000/-

Ijumaa, 17 Machi 2017

KILIMO BORA CHA TANGAWIZI


Tangawizi ni moja kati ya aina za mazao ya viungo ambayo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Zao hili kwa lugha ya kigeni linafahamika kama Zingiber officinale.

UDONGO NA KUSTAWI

Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha milimita 1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi

joto 20°C-25°C. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usio-tuamisha maji.

AINA

Mpaka hivi sasa hakuna aina rasmi za tangawizi ambazo zimeainishwa na kuthibitishwa kuzalishwa nchini Tanzania. Pamoja na hili, kuna aina tatu za tangawizi ambazo zimezoeleka kuzalishwa na wakulima hapa nchini. Aina hizo ni Tangawizi nyeupe maarufu kama  White Africa au  Jamaica, Cochin

(flint), na Bombay.

Tangawizi inayopandwa katika sehemu tambarare huwa laini zaidi

kuliko inayozalishwa kwenye maeneo ya milima, ambayo huwa ngumu na kuwa na nyuzi nyingi zaidi.

NAFASI

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita 5-10. Unaweza kupanda sehemu yenye

miti au migomba ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji mara

kwa mara endapo mvua inakosekana hadi kufikia mwezi mmoja kabla ya kuvuna.

MATUMIZI

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji kama vile chai, soda, juisi, vilevi na kadha-lika. Kuna aina mbalimbali za vyakula ambavyo pia hutengenezwa kwa kutumia tangawizi kama vile mikate,

biskuti, keki, nyama za kusaga, achari

na kadhalika.

Tangawizi pia hutumika  katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi. Hali kadhalika tangawizi

hutumika katika kutengeneza vipodozi vya aina mbalimbali vile

kama poda

MBEGU NA NAMNA YA KUPANDA

Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu. Vipande vya tangawizi huhifadhiwa mahali pakavu penye ubaridi ili kuweza kuchipua.

Machipukizi hukatwa urefu wa sen-timita 2.5-5. Baada ya hapo, unaweza kupanda machipukizi hayo kwenye matuta au shambani kawaida endapo eneo lako ni tambarare.

Baada ya kupanda, tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.

MATAYARISHO

Ondoa takataka zisizohitajika shambani. Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekari moja.

PALIZI

Katika kipindi cha wiki mbili, magugu huanza kuchomoza kwa kuwa udongo huwa na unyevu kwa wingi. Fanya palizi mara majani yanapojitokeza.

Endelea kung’oa magugu na kuweka shamba katika hali ya usafi hadi wakatiwa kuvuna.

KUPANDA

Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati  Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futimbili na majani yake ni membamba  marefu, ambayo hufa kila mwaka

yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

MAGONJWA NA WADUDU

Madoa ya majani:  Yanayosababishwa na viini vya magonjwa viit-

wavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.

Kuoza kwa tunguu: Kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp.

Mizizi fundo: Inasababishwa na Meloidegyne spp.

UVUNAJI

Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapo-geuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa.

Tangawizi itakayohifad-hiwa ivunwe mapema kabla haijako-maa kabisa, na ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi

hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, yanaweza kuwa kiasi

cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa hekari moja.

Alhamisi, 16 Machi 2017

JIKINGE AU JITIBU ‘PRESHA YA KUSHUKA ’ KWA CHAKULA


Presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu (hypotension) hali hii inatokea pale msukumo wa damu unapakua mdogo na dhaifu, halo ambayo husababisha viungo muhimu katika mwili (major organs) kushindwa kupokea kiasi cha damu na oksijeni kinacho jitosha

DALILI ZA MTU MWENYE PRESHA YA KUSHUKA

Mtu mwenye ugonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara husumbuliwa na uchovu, mwili kukosa nguvu, kuwa mnyonge na kusikia kizunguzungu. Hali hii hutokea baada ya mzunguruko wa damu kwenye mishipa kuwa mdogo kutokana na kupungua kwa msukumo wa damu hivyo viungo kama moyo, ubongo na viungo vingine kupungukiwa au kukosa damu kabisa.

SABABU ZA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa mujibu wa wataalamu wetu wa masuala ya lishe, sababu kubwa inayochangia ugonjwa huu ni ukosefu wa virutubisho mwilini kunakosababishwa na ulaji usio sahaihi. Mtu anapokuwa na upungufu wa protini, vitamin C au moja kati ya Vitamin B hupatwa na tatizo hili. Aidha, ugonjwa wa presha ya kushuka, wakati mwingine husababishwa na kuvuja taratibu kwa damu mwilini kupitia kwenye utumbo, figo au kibofu. Mbali na matatizo hayo, pia hasira, kupatwa na msongo wa maisha na mawazo mengi, kunaweza kusababisha presha ya kushuka pia.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa mujibu wa watatifi wa vyakula, wamegundua kuwa juisi ya Bitiruti (beetroot) ina saidia sana mgonjwa anayesumbuliwa na ugonjwa huu. Bitiruti ni aina fulani ya viazi pori ambavyo vinabapatikana kwenye masoko mbalimbali nchini. Mgonjwa anashauriwa kutengeneza na kunywa kikombe kimoja cha juisi hiyo kutwa mara mbilli na anaweza kuona mabadiliko ndani ya wiki moja tu.

KUOGA MAJI YA CHUMVI
Dawa nyingine inayoweza kutoa nafuu na ya haraka kwa mgonjwa wa presha ya kushuka ni kuoga kwa kujiloweka kwenye maji ya chumvi maalum. Chukua kilo moja na nusu ya chumvi, kisha weka kwenye beseni kubwa la maji ya uvuguvugu, koroga kisha ingia ndani ya beseni hilo na ukae kwa dakika 10 hadi 20. Fanya hivyo muda mfupi kabla ya kwenda kulala na usipatwe na baridi.

VIRUTUBISHO KAMA TIBA
Protini, Vitamin C na Vitamin zote za kundi B, vimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga au ahueni kwa wagonjwa wa presha ya kushuka. Mlo kamili wowote ulioshehemi vitamini B na virutubisho vingine, ni muhimu kuliwa na mgonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara.

Matumizi ya chumvi nyingi kwa mgonjwa wa presha ya kushuka nayo ni muhimu. Mgonjwa anashauriwa kula vyakula vyenye chumvi nyingi. Aidha, anaweza kunywa maji yaliyochanganywa nusu kijiko cha chumvi kila siku, hadi hapo kiwango cha presha yake kitakaporejea katika hali ya kawaida.

Ili kuliondoa tatizo la presha ya kushuka moja moja, mgonjwa wa presha ya kushuka anatakiwa kuzingatia ulaji wa matunda kwa kiasi kikubwa. Kwa kuanzia, anatakiwa kula mlo wa matunda-matunda tu kwa muda wa siku tano mfululizo, huku akila mlo huo mara tatu kwa siku ukipishana kwa umbali wa masaa matano.

Baada ya hapo, mgonjwa huyo anaweza kubadilisha mlo na ukawa wa matunda na maziwa kwa muda wa wiki mbili hadi tatu. Na baada ya hapo, anatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vyenye virutubisho vya kutosha ili kuimarisha mfumo wa damu mwilini. Na hii ndiyo iwe staili yake ya maisha kila siku, bila kusahahu mazoezi mepesi mepesi, yakiwemo yale ya kuvuta pumzi na kushusha.

MAAJABU YA MAFENESI ( ARTOCARPUS HETEROPHYLLUS LAM)


MAFENESI au Jackfruits kwa lugha ya kiingereza na majina mengine Langka na Nangka ni matamu kwa ladha yake. Lakini pia yana umuhimu katika mwili wa binadamu.

Hakuna anayejua vizuri asili ya mafenesi lakini inaaminika asili yake ni katika misitu ya mvua nyingi ya Magharibi ya ghats (western ghats).

Lakini kwa sasa inalimwa katika nchi za india, Burma, Sri lanka, China, Malaya, East in indies, Qeens land, Maturities, Hawaii, Suriname, Brazil, Kenya, Uganda na Tanzania,

Na nchini Tanzania hulimwa Pemba, Unguja, Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga na Mbeya(Kyela) nk.

Na sehemu zinazotumika ni majani, matunda, utomvu, mizizi na magamba. Na mfenesi unaweza kukua hadi kufikia kimo cha mita 20.

Mafenesi yana vitamin B1 na B2, vitamin C, flavonoids na ni chanzo kizuri cha carotenoids na Potassium nk. Katika nchi kama Thailand majani machanga na maua machanga ya kiume hupikwa kama mboga. Matunda yaliyoiva hulimwa yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa na nazi au hutengeneza ice cream, chatine(chutney), jam, jeli, (jelly) na pesti.

Mfenesi una faida nyingi tukianzia na majani hutibu homa  magonjwa ya ngozi majipu, vidonda na kisukari. Tunda lina wingi wa vitamin C ambayo kiafya inasaidia kuongeza kinga ya mwili, tunda hili linasaidia kupunguza mafua, kifua na homa. Vitamin C hiyo husaidia kuondoa sumu mwilini na kuukinga mwili na maradhi pale linapotumiwa ipasavyo.

Fenesi pia linasaidia kuupa mwili nguvu kwani lina madini ya wanga na sukari ambayo husaidia kuupa mwili nguvu kwa haraka. Fenesi linaweza kuondoa sumu mwilini hivyo linakinga na saratani za aina mbalimbali kama ile ya mapafu. Mdomo na kinywa  na tumbo. Fenesi hutia nguvu mwili na kwenda haja vizuri. Kwa wale wenye matatizo ya shinikizo la damu, Fenesi ni tiba nzuri kwani ina madini ya potassium ambayo husaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza uwezekano wa kupata  shinikizo la damu na kukuondoa katika hatari ya kupata kiharusi. Mizizi yake hutibu homa, kuharisha, magonjwa ya ngozi  na asthma. Utomvu wake ukichanganywa na siki hutibu tambazi (abscesses), kuumwa na nyoka na uvimbe wa tezi (glandular) nk. Magamba yake hutibu vidonda kwa kuweka kibandiko (poultices)

Mbegu zake zikikaangwa huongeza tendo la kujamiiana.

Watanzania tuanze kula fenesi baada ya kula husaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula kwa sababu ni tunda muhimu na linasaidia pia kuzuiwa kuvimbiwa. Pia kwa wenye matatizo ya macho na kutokuona vyema, tunda hili ni mkombozi mkubwa  kwani lina wingi wa vitamin C ambayo huongeza kiwango cha kuona (uoni), pia lina uwezo wa kuondoa sumu, hufanya kazi katika retina na kuifanya iwe imara.

 

Jumatano, 15 Machi 2017

Chakula cha mtu mwenye Vidonda vya Tumbo



Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo na leo tunaendelea kuangalia chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kupunguza uzalishaji wa asidi tumboni au mwilini kwa ujumla.

Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa ni muhimu.

Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4 mpaka 6 za matibabu.

Mtu mwenye vidonda vya tumbo ni mtu mwenye asidi nyingi mwilini kuliko alkalini, hivyo anatakiwa kupendelea zaidi kula matunda na mboga za majani. Anahitaji zaidi ukijani mwilini mwake. Pia apendelee kula ugali wa dona kuliko ugali wa sembe na inashauriwa pia kupunguza kula wali.

Kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo ni maji. Hakikisha unakunywa kila siku maji glasi 8 hadi 10.

 

MAZOEZI MAALUMU KWA ANAYESUMBULIWA NA MIGUU KUWAKA MOTO AU ASIDI KUZIDI MWILINI

Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5


Kisha simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5

Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.


Hapa chini nimekuwekea jedwali la jumla la vyakula na vinywaji vyenye asidi sana, asidi ya kati na alkalini sana, vile vya kuviepuka ni vile vyenye asidi sana, orodha itaendelea kuboreshwa;

Chakula cha mtu mwenye Vidonda vya Tumbo

Mayai na bidhaa za maziwa

  • Alkaline: mtindi

  • Neutral: mtindi mtupu (plain Yogurt ),

  • Acid: siagi, krimu, mayai, jibini ngumu (Hard Cheese), Ice Cream, jibini ya kiwandani (Processed Cheese), maziwa


Vyakula jamii ya maharage

  • Alkaline: Lima, njegere, Snap, String

  • Neutral: Soya

  • Acid: Black, Garbanzo, Kidney, dengu


Vyakula jamii ya karanga

  • Alkaline: lozi, Nazi freshi (fresh)

  • Neutral:

  • Acid: Brazil, korosho, Nazi kavu (dried coconut), Macadamia, karanga, Pecan, Pistachio, Walnut


Mboga za majani

  • Alkaline: asparaga (Asparagus), kiazisukari (Beets), brokoli (broccoli), kabeji, karoti, Koliflawa (aina ya kabichi – Cauliflower), figili (Celery), tango, mwani (Kelp), saladi (Lettuce), uyoga, vitunguu, kotimiri (Parsley), Bell Peppers, viazi ambavyo havijamenywa (with skin), boga (Squash), nyanya

  • Neutral: Horseradish, Rhubarb, Sauerkraut

  • Acid: Spinachi iliyopikwa, viazi ambavyo vimemenywa (no skin Potato), achali


Matunda

  • Alkaline: tufaa (Apple), parachichi, tende, mtini, zabibu, balungi, Kiwi, Limau, ndimu, embe, tikiti maji, chungwa, mpichi, Pears, Stroberi

  • Neutral:

  • Acid: Blueberry, Cranberry, plamu (Plum), plamu kavu (Prune)


Vinywaji

  • Alkaline: Maji ya limau, Chai ya tangawizi

  • Neutral: Maji

  • Acid: Chai ya rangi, Bia, kahawa, vinywaji vyenye kafeina, juisi za viwandani (processed), Liquor, Soda, Wine


Viongeza utamu

  • Alkaline: Asali mbichi (Raw Honey), sukari mbichi (Raw Sugar), Stevia

  • Neutral:

  • Acid: Viongeza utamu vyote vya kutengenezwa (Artificial Sweeteners)


Nyama

  • Alkaline:

  • Neutral:

  • Acid: Nyama ya ng’ombe, kuku, Samaki, mbuzi, batamzinga, nyama ya nguruwe, Sungura


Mafuta

  • Alkaline: mafuta ya mbegu za katani

  • Neutral: mafuta ya lozi, Canola, mafuta ya nazi, mafuta ya mahindi, Margarine, mafuta ya zeituni, Safflower, mafuta ya ufuta, mafuta ya Soya, mafuta ya alizeti

  • Acid:


Vitafunwa & nafaka

  • Alkaline: Amaranth, Millet, Quinoa

  • Neutral:

  • Acid: Barley, Buckwheat, Oats, mchele, Rye, Spelt, ngano, Pasta (vyakula jamii ya tambi), biskuti


Mbegu

  • Alkaline: Alfalfa (sprouted), chia (sprouted), Sesame (sprouted)

  • Neutral:

  • Acid: boga, alizeti, ngano



Ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili): kanuni bora za ufugaji





Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.

Dondoo ya 1

Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku

Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;

  1. Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.

  2. Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.

  3. Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.

  4. Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.

  5. Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.

  6. Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.

  7. Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.


Dondoo ya 2

Magonjwa na kinga kwa kuku wote

Ndui ya kuku

Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.

Mdondo/kideri

Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.

Ukosefu wa vitamini A

Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.

Kosidiosisi

Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.

Viroboto, chawa na utitiri

Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.

Minyoo

Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.

Dondoo ya 3

Chakula cha ziada

  1. Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.

  2. Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).

  3. Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.

  4. Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.

  5. Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.

  6. Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.


Dondoo ya 4

Utotoleshaji wa vifaranga

Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.

Sifa za jogoo bora

  1. Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.

  2. Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.


Sifa za tetea bora

Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.

Uhifadhi wa mayai

  1. Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.

  2. Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.

  3. Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.

  4. Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.

  5. Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.

Kuatamiza mayai


  1. Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.

  2. Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.

  3. Mayai ya kuatamiza yasizidi wilki 2 toka kutagwa.

  4. Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.

  5. Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti


Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja

  1. Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;

  2. Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.

  3. Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.


Dondoo ya 5

Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo

Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine

  1. Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasinde mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.


Chanjo ya mdondo kideri/lufuo

Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.

Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3

Kinga dhidi ya kosidiosisi

Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.

  1. Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.

  2. Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba

  3. Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;


Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho

  1. Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.

  2. Usichanganye kuku na bata katika banda moja

  3. Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.

  4. Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.

  5. Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.

  6. Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.

  7. Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.

  8. Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.

  9. Soma maelezo haya mara kwa mara na ufanye yalioelekezwa.

  10. Washirikishe wengine katika kaya yako ili nao wajifunze na kufanya hivyo kukuza ufugaji na kipato cha familia.