• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Jumatatu, 13 Agosti 2018

HIZI NDIZO SABABU ZA KUKU WAKO KUDONOA MAYAI NA KUDONOANA


Kati ya mambo ambayo mfugaji anatakiwa kuwa nayo makini ni pamoja na tabia za kila siku za mifugo yake. Kuna wakati kuku wanakuwa na tabia za kudonoa na kula mayai,pia kudonoana wenyewe kwa wenyewe. Tabia hii si nzuri na si ya kawaida. Hizi hapa chini ni sababu zinazopelekea kuku kuwa na tabia hizi:

SABABU ZA KUKU KULA MAYAI.

1. Ukoo- Hapa utakuta ndo ukoo/uzao wao wanatabia ya kula mayai hivyo kuku hufanya muendelezo wa kula mayai,

2. Kuto kupata chakula cha kutosha- Hii ni moja ya sababu kubwa kabisa inayo pelekea kuku kula mayai,chakula kikiiwa kichache hawashibi hupeleka kutafuta njia mbadala ya kushiba. 

3. Kukosa madini joto- Hii inaweza kuwa ndo sababu kuu ya kwa nini kuku wanakula mayai, kuku wakikosa madini joto ni lazima wale mayai na hata kulana wao wenyewe, na jua kwamba kwenye yai kuku huwa anatafuta lile ganda la juu pekee sema anapo donoa na kulipasua yai hujikuta anakula na ute na kiini ila yeye lengo lake hasa ni ganda la juu.

 4. Kuku kutagia sehemu nyeupe sana yenye mwanga mkali upelekea kuku kula mayai,kuku anapenda kutagia sehemu fichifichi yenye mwanga hafifu kidogo ndo anakua huru zaidi kutaga.

5. Mayai kukaa muda mrefu bila kukusanywa baada ya kutaga- Hapa ni kwamba mayai yanapo kaa muda bila kukusanywa na kama yapo sehemu ya wazi ni rahisi wao kudonoa.

6. Lishe mbaya-kuku akipata lishe mbaya ya chakula humpelekea kudonoa chakula,kuku anapaswa kupata chakula chenye virutubisho vyote.

7. Nafasi ndogo-kuku wanapaswa kupata nafasi kubwa yakupumzika na kulia chakula.

8. Vyombo vichache-bandani unapaswa kuwa na vyombo vya chakula na maji vya vyakutosha kuondoa kusukumana na kutokula kwa raha.

9. Kukosa shughuli yakufanya-kuku wakila wakishiba unapaswa kuwafungia majani km kabeji ili wawe bize mda wote.

NAMNA YA KUZUIA KUKU KUDONOANA AU KULA MAYAI 

1. Chakula cha kutosha ni muhimu sana, ili kuwafanya wasitake kula mayai ili kushiba.

 2. Mayai yakusanywe mara tu anapo taga na usiyaache muda mrefu bandani. 

3. Sehemu ya kutagia iwe na giza la kutosha ili kufanya kuku ashindwe kuona yai alilo taga.

4. Madini joto ni muhimu sana. 

5. Kuku wenye tabia za kula mayai unaweza chinja au kuuza. 

6. Kuweka idadi ya kuku inayolingana na sehem ulionayo.

 7. Usizidishe mwanga. 

8. Banda liwe safi.

9. Weka vyombo vya kutosha. 

10. Wape lishe bora

11. Wape kuku shughuli kwa kuwawekea bembea na sehemu ya uwazi kwa ajili ya mazoezi. 

12. Kata midomo ya juu.

13.Epuka ukoo wenye tabia hizo.

Kwa leo naishia hapa,nakutakia mafanikio mema kwenye ujasiriamali wako, Mungu awabariki sana.
⁠⁠⁠