• TANZAKILIMO TANZANIA

    Pata taarifa sahihi kuhusu kilimo na ufugaji,kwa weledi wa hali ya juu

  • WATAALA WA KILIMO NA UFUGAJI

    Tunakupatia ushauri wa kitaalam katika maswala yote ya kilimo na ufugaji,toka kwa wataalam wetu waliobobea kwenye nyanja nzima ya kilimo. Wasiliana nasi kwa simu namba +255 675 117 151.

  • UNATAFUTA MASOKO YA MAZAO YAKO? UNATAFUTA MAZAO YA KUNUNUA?

    Tanzakilimo inakuunganisha na wakulima/wanunuzi na wadau wote wa maswala ya kilimo. Wasiliana nasi leo tukuunganishe na wadau....

Jumanne, 8 Februari 2022

kilimo cha ngano na faida zake

 

kilimo cha ngano na faida zake



Utangulizi:

Hapa nchini, zao la ngano linalimwa zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, na Manyara, kwa upande wa kaskazini na Iringa, Mbeya na Rukwa kwa upande wa kusini. Ngano ni zao la tatu la umuhimu la chakula hapa nchini. Bidhaa mbalimbali za chakula zinazotengenezwa na ngano ni Pamoja na mikate, biskuti, keki, chapati, mandazi, n.k.


Faida za kilimo cha Ngano:

1. Mbegu yake hutumika kama chakula

2. Zao la ngano ni zao la kibiashara hivyo huongeza kipato kwa mkulima

3. Unaweza ukaongeza thamani kwa kuchakata ngano na kutengeneza bidhaa mbalimbali

4. Husaidia kwenye kilimo mzunguko hivyo kutunza virutubisho kwenye shamba


Udongo:

Ngano ni zao linalostawi vizuri katika udongo;

1. Unaopitisha maji vizuri na wenye wastani mzuri wa kiasi cha pH kati ya 5.5 mpaka 6.5.

2. Wenye unyevu wa kutosha

3. Wenye virutubisho vya kutosha vya madini kama nitrogen, fosforasi na calicium


Zao la ngano hustawi vizuri katika maeneo ya miinuko (wastani wa mita 1,200) kutoka usawa wa bahari, maeneo ya kati (usawa wa mita 900) na maeneo ya chini ya mita 900 kutoka usawa wa bahari. Hakikisha unapima udongo wa shamba lako kabla ya kuanza kilimo ili ujue afya ya udongo. Hii itakusaidia kujua ni aina gani ya mbolea utahitaji na kwa kiasi gani. Kufanya hivi kutachangia kuongeza ufanisi na upatikanaji wa mavuno mazuri.


Mbegu

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za zao la ngano zinazotumika hapa nchini. Aina hizi za mbegu zimethibitishwa na kufanyiwa majaribio na vituo vya utafiti wa kilimo hapa nchini na kuthibitika kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali. Katika kuchagua mbegu bora ni vizuri kuzingatia sifa zifuatazo;

1. Mbegu zinazozaa vizuri

2. Mbegu Zinazowahi kukomaa shambani

3. Mbegu zinazovumilia ugonjwa

4. Mbegu zinazovumilia ukame


Miongoni mwa aina za mbegu zinazofanya vizuri ni pamoja na Juhudi, Lumbesa, Sifa, Tai, Mbuni, Merina, Ngoli, Shangwe, Trophy, Selian 87, Njombe 7 na Mamba.

Mbolea:

Kiasi cha juu cha kilo 50 za mbolea za chumvi chumvi zinaweza kuhitajika katika eneo la ekari moja. Unaweza kuchanganya mbolea ya chumvi chumvi na samadi ili kuongeza ufanisi. Zipo aina mbalimbali za mbolea za chumvi chumvi. Pia unaweza kutumia mboji kurutubisha shamba lako. Ain ana kiasi cha kutumia itategemea na majibu ya vipimo vya udongo katika shamba lako.


Viuatilifu

Magonjwa na wadudu wanaweza kushambulia mimea ya ngano ikiwa shambani. Unashauriwa kukagua shamba lako mara kwa mara ili kuangalia maendeleo ya mimea yako. Endapo kutatokea ugonjwa au wadudu ni vema ukamuona mtaalaamu wa kilimo kwa msaada Zaidi ya utambuzi wa ugonjwa au aina ya wadudu waliopo na hivyo ukapatiwa ushauri wa aina na kiasi cha kiuatilifu cha kutumia ili kudhibiti tatizo hilo.



Mavuno:

Kiasi cha mavuno hutegemea na aina ya mbegu utakayotumia. Endapo utazingatia matunzo mazuri, unaweza kuzalisha kiasi cha 3.5 mpaka 5.5 tons/hecter.